Mwanamuziki mashuhuri Diamond Platnumz amewaeleza mashabiki wake kuwa, wampe muda kidogo maana ana jambo kwao baada ya kumalizana na vyombo vya habari.
Mmiliki huyo wa Wasafi TV na Wasafi FM pamoja baadhi ya vituo vingine vya habari pamoja kampuni ya kuekeza ya Wasafibet, ameeleza kuwa amefanya mengi upande wa vyombo vya habari na hivyo mashabiki hawana budi kusubiri kurejea kwake katika muziki kama iliyo ada yake.
Katika mtandao wake wa Instagram, ‘Simba’ kama anavyojiita alisema kuwa, hadhani kuwa kuna jambo limesalia katika upande wa muziki. “ Nadhani kwenye Media nimemaliza, niendelee na shughuli zangu zingine sasa, au kuna pahala pamesalia?” Aliuliza Diamond.“ Ooh! THE SWITCH, MASHAMSHAM, WEEKEND SHOWS, WASAFI TV, & SINGELI SHOW KWA RADIO ...Kwenye muziki mnisubiri kidogo, bado mna jambo langu kwanza! ” Aliendelea.
Kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Charts Tanzania, ulionesha kuwa nyota huyo wa kibongo alikuwa kileleni mwa jedwali katika nyimbo zilizotazamwa sana kwenye mtandao wa You Tube, huku akiwa ametazamwa na watu 33.3M mwezi uliopita. Hii ni kutokana na kibao chake za Zuwena mwaka huu, ambacho kilitazamwa sana.
Bosi huyo wa WCB pia wimbo wake akimshirikisha Zuchu Mtasubiri sana ni miongoni mwa nyimbo zinazoendelea mlimlikizia umaarufu siku baada ya siku na kufanya nyimbo zake kupendwa na watu wengi katika eneo la Afrika Mashariki.