Meneja wa WCB Wasafi ambaye pia ni mbunge Babu Tale ameweka wazi kuhusu uvumi ambao umekuwa ukiendeshwa kwa muda mrefu kwamab msanii ambaye ana mkataba ndnai ya lebo hiyo akitaka kuuvunja mkataba ni sharti alipe shilingi sio chini ya milioni 500 za Tanzania, sawa na millioni 30 za Kenya.
Tale alidhibitisha kwamba ni ukweli na kutaja sababu kuu ikiwa ni kurudisha kiasi ambacho uongozi wa lebo unawekeza kwenye makuzi ya msanii huyo, kwani muziki kwao siku zote wanauangalia kwa taswira ya kibiashara Zaidi kuliko kuburudisha.
“Ndio ni kweli, ni utaratibu kwa sababu mimi siwezi kuchunga kinyago halafu mtu anakuja kukichukua bure tu. Thamani yake imeshakuwa kubwa, biashara yake ishakua sasa tunaachanaje?” Tale alisema sababu ya kumtoza msanii hela hizo ndefu kabla kuvunja mkataba.
Babu Tale alisema kuwa biashara ya kumtengeneza msanii ni ngumu na inahitaji jitihada nyingi, na kwa hivyo akishakua na afikie kiwango cha kutaka kuondoka, sharti afuate utaratibu wa kumrudishia mwekezaji faida zake kabla ya kuruhusiwa kuondoka.
Alisema kwamba msanii Rayvanny alilipa kiasi ambacho si chini ya milioni 500 na hakulalamika wala kuumia kwani alikuwa anaelewa utaratibu wa kuvunja kandarasi kutoka Wasafi.
“Biashara ya kumtengeneza msanii ni safari ndefu sana. Na hela hizo tunawatoza ni kidogo ukilingansiha na kile ambacho tumetengeneza ndani yake. Ila unachukua tu ili uone kwamba na mimi nimefunga duka, ni sehemu ya hasara niliyoipata. Yeye ndio anapata faida kubwa kwa sababu ya pale ulipomfikisha,” alisema.
Meneja huyo wa muda mrefu alisema kuwa uongozi wa lebo ndio hushikilia kaunti zote za mitandaoni za wasanii wote.
“Huwa tunashikilia akaunti zote yaani hawezi kukuruka, ni biashara. Kila kitu ni cha kwako kwa sababu wewe ndio umewekeza, umewekeza hela.”
Tale alifunguka kwamba kwa mfano leo hii Zuchu akataka kuondoka Wasafi, atalazimika kuzama mfukoni Zaidi ili kutengana na kiasi kisichopungua bilioni 5 za Tanzania, katika kile alisema kuwa wameshamkuza hadi kuwa msanii mkubwa wa kike katika mataifa 7 ya Afrika Mashariki.
“Siku moja Zuchu akitaka kuondoka atatulipa bilioni 50. Maana hapo tumuonye mapema. Sababu thamani yake ni kubwa, ni mwanamuziki wa kike anayefanya vizuri kote Afrika Mashariki. Mataifa 7 anadfanya vizuri. Hatuwezi kumuuza kwa milioni 500, yule ni wa bilioni 5, au 10, bora tuweke ndani tujue moja,” Tale alisema.