logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Najua mamangu na mtoto wangu Ifeanyi wanadensi kwa nyimbo zangu mbinguni - Davido

"Mwanangu huko juu ananitazama, asingependa niwe kama mnyonge.”

image
na Davis Ojiambo

Burudani13 June 2023 - 10:02

Muhtasari


  • • Davido alifichua haya katika mahojiano na Podcast ya Million Dollar Worth Of Game, iliyochapishwa Jumatatu.
  • • "Watu wengi walidhani tutaangusha albamu na kutakuwa na huzuni nyingi, wanaume tuliwapa bangers baada ya bangers.” - Davido.

Mwimbaji nyota kutoka Nigeria, David Adeleke, almaarufu Davido, amesema kuwa ingawa watu walitarajia nyimbo nyingi za kusikitisha wakati albamu yake ya ‘Timeless’ ilipodondoka, aliimba vibao vyenye furaha na tafrija, kwa sababu alijua mama yake na mwanawe wanacheza mbinguni.

Davido alifichua haya katika mahojiano na Podcast ya Million Dollar Worth Of Game, iliyochapishwa Jumatatu.

Alisema, “Nilijitazama kwenye kioo nikasema, bruh, mbali na mimi kuwa juu yangu tu najua nina watu wengi wanaonipenda, watu wengi wanaonitegemea, mwanangu huko juu ananitazama, asingependa niwe kama mnyonge.”

Msanii huyo alisema kuwa ngoma nyingi alizoimba kwenye albamu hiyo ambayo aliitoa miezi michache kufuatia kifo cha mwanawe wa pekee,zilihimizwa na marehemu Ifeanyi, mwanawe kwaki anajua fika kwamba ana jukumu la kusimama upande wa faraja na mamake, ambaye ni mume wake na pia kuonesha dunia ujasiri wa kuweza kustahimili mambo magumu licha ya changamoto na mapigo kama hayo ya kufiwa.

"Mbali na mimi kuwa na nguvu kwa ajili ya mama yake, ambalo ni jukumu langu la msingi, lazima niwe na nguvu kwa ulimwengu.”

"Watu wengi walidhani tutaangusha albamu na kutakuwa na huzuni nyingi, wanaume tuliwapa bangers baada ya bangers.”

‘'Mwanangu anacheza, mama yangu anacheza mbinguni pia. Ili watu waone kuwa inawezekana. Sio kwamba ninamtakia mtu yeyote, singetamani kamwe kwa adui yangu, unaelewa?”

"Lakini kuweza kusimama tena na kuweza kufanya kazi. Ni Mungu tu, huwezi kuniambia chochote, ni Mungu tu.”Msanii huyo alimaliza kwa sauti iliyojawa na uchungu wa kiume.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved