Mwimbaji maarufu wa Nigeria, David Adeleke, almaarufu Davido, hatimaye amekiri kupata mtoto na babymama wa nne anayedaiwa kuwa ni Larissa London, kulingana na video ambayo imevijishwa mitandaoni.
Mwimbaji huyo wa ‘Omo Baba Olowo’ alisema kuwa ana mtoto wa kiume anayeitwa Dawson ambaye anaishi London.
Alisema hayo katika mahojiano ya hivi majuzi ya podcast moja.
Davido alisema aliwaita binti zake, Imade na Hailey jina la marehemu mama yake, akisisitiza kuwa binti yake wa pili, Hailey ni mfano wa mama yake.
Alisema, “Niliwaita wote wawili [binti zangu] kwa jina la mama yangu. Hailey, yeye ni mfano halisi wa mama yangu; binti yangu wa pili, yeye ni kama mama yangu. Ni wazimu. Ni kama aliingia ndani yake.
“Halafu pia nina mtoto wa kiume. Jina lake ni Dawson. Anaishi London hivi sasa."
Radio Jambo inakumbuka kwamba Davido alipoteza mwanawe wa kwanza, Ifeanyi Adeleke katika ajali ya kidimbwi cha kuogelea katika makazi yake ya Kisiwa cha Banana Oktoba mwaka jana.
Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya wanamitandaoni wanahisi kwamba msanii huyo amekuwa mzungumzaji sana, huku akiendelea kuweka wazi mambo ya ndani ya familia yake, jambo ambalo hakuwa analifanya hapo awali.
Wengine pia walihisi kwamba msanii huyo katika kuzungumzia watoto ambao amewazaa na wanawake wengine wakati mtoto ambaye alizaa na mpenzi wake Chioma ameshafariki ni sawasawa na kuathiri kwa njia hasi hisia za Chioma ambaye bado hajafanikiwa kupata mtoto mwingine.
Ikumbukwe wiki jana iliripotiwa kwamba babymama wa kwanza alitishia kuifuta tattoo ya jina la msanii huyo kutoka kwa mwili wa binti ambaye walizaa pamoja, katika kile alieleza kuwa Davido huwa hamsaidii katika matunzo na mahitaji ya kumlea mwanao.