logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Azziad ajiondoa studioni baada ya kuulilzwa sababu ya kubatilishwa kwa uteuzi wake

Azziad Nasenya alijiondoa kwenye mahojiano na mtangazaji mmoja wa radio.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 June 2023 - 09:54

Muhtasari


  • • Pindi tu mtangazaji huyo alipomuuliza Azziad swali hilo, soshalaiti huyo alisema kuwa swali hilo halikuwa sawa na lilikiuka maelewano yao wa hapo awali.
Azziad Nasenya akiwa katika Ikulu ya Nairobi katika uzinduzi wa Talenta Hela.

Mwanatiktok maarufu, Azziad Nasenya alijiondoa kwenye mahojiano na mtangazaji mmoja wa radio baada ya kuulizwa kuhusu uteuzi wake kwenye baraza la Talanta Hela kubatilishwa.

Pindi tu mtangazaji huyo alipomuuliza Azziad sababu ya uteuzi wake katika baraza hilo, alionekana kukerwa na swali hilo na kuondoka nje ya studio akisema kuwa swali hilo halikuwa sawa na na tayari walikuwa wameelewana hapo awali.

Tukio hilo, lililonaswa moja kwa moja kwa TikTok, lilizua mjadala mkali kuhusu mipaka ya wanahabari katika juhudi zao za kuwaharifuu wasikilizaji.

Aidha mwanahabari huyo alitetea msimamo wake wa kumuuliza swali hilo akisema kuwa ilikuwa wajibu wake kama mwandishi wa habari kuuliza maswali. 

Mtangazaji huyo alidai kuwa swali hilo tata lilikuwa muhimu kwa mahojiano yao kuwa na maana na kutoa habari muhimu kwa wasikilizaji.

Hilo swali si baya, kwa sababu kusema ukweli mimi ni mwanahabari na kama singeuliza swali hilo, mahojiano hayo hayangekuwa na umuhimu wowote kwa wasikilizaji."

Mwanahabari huyo alihisi kuwa kama Azziad hakutaka kuzungumzia swala hilo basi angesema hivyo tu kwa urahisi akiwa hewani kuliko kuondoka katikati ya mahojiano hayo.

Tukio hilo lilibua hisia mseto mitandaoni, wengine walisema kuwa msasa wa Mwende ulikuwa muhimu ili kutoa picha kamili, wengine waliona kuwa mtangazaji huyo alivuka mstari wa faragha na heshima kwa matakwa ya mhojiwa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved