logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maelfu ya watu wamiminika Jacaranda usiku wa manane kumkaribisha Pasta Ezekiel

Ezekiel alisema kuwa Nairobi ndipo alipoanzia huduma yake na amerudi kuanzia huko tena.

image
na Davis Ojiambo

Burudani01 July 2023 - 10:14

Muhtasari


  • • Ezekiel alisema kuwa Nairobi ndiko alikoanzia huduma yake katika uwanja wa Jacaranda na kwa mara nyingine kuonesha furaha yake kurudi kuanzia huko tena.
Pasta Ezekiel katika uwanja wa Jacaranda

Maelfu ya wakaazi wa jiji la Nairobi usiku wa Ijumaa walifurika katika uwanja wa Jacaranda kumkaribisha mchungaji Ezekiel wa New Life Church huko Mavueni kaunti ya Kilifi.

Mchungaji Ezekiel anatarajiwa kuongoza mkusanyiko mkubwa wa ibada katika uwanja huo wikendi hii, ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kuachiliwa kwa dhamana katika kesi ambayo inalenga kuchunguza uhusiano wa kanisa na mahubiri yake na mchungaji Paul Mackenzie ambaye anamulikwa kwa kuwashrutisha waumini kujinyima chakula na maji hadi kufa ili kumuona Mungu.

Katika video ambazo zimesambazwa mitandaoni, Ezekiel alionekana akizungumza na watu hao waliofurika kila mmoja alitafuta nafasi ya kujipenyeza ili kumuona, naye alishangaa akiwauliza ni saa ngapi walikuwa wanalenga kulala kwani ulikuwa ni usiku sana.

Ezekiel alikumbuka kwamba uwanja wa Jacaranda ndiko alikoanzia ibada yake ya mikutano ya maombi miaka kadhaa iliyopita na hatimaye amerudi.

“Mimi swali mmoja ninauliza, mnalala saa ngapi? Tunakesha? Lakini Mungu ametupa crusade Nairobi Jacaranda. Hapa ndio tulianzia, na mara nyingine Mungu ametupa neema ya kuanzia tena huku,” Ezekiel alisikika akisema huku akimnyoshea kidole jamaa mmoja na usema kuwa amewahi muona.

Ezekiel alisema kuwa baada ya ibada zake kupigwa breki kidogo kutokana na mchakato wa kesi, amerudi tena kwa kishindo ambapo mkutano huo mkuuutachukua simu mbili katika uwanja huo.

Mchungaji huyo aliwapongeza watu wa Nairobi akisema kuwa alishangaa kuwaona watu wengi wakiwa macho usiku wote huo bila kulala kama wengine.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved