Mkuzaji maudhui kwenye mtandao wa TikTok kwa mara ya kwanza amefichua jinsi alivyopata virusi vya UKIMWI, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuweka wazi kupitia ukurasa wake TikTok kwamba yeye ni mwathirika wa virusi vya HIV.
Katika mahojiano ya kipekee na Oga Obinna, Chira alisema kwamba alikwenda jijini Mombasa katika tafrija Fulani ambapo kabla ya tafrija yenyewe, rafiki yake ambaye akikuwa anasoma chuo kimoja jijini humo alimualika kwake.
“Nilienda Mombasa, nilialkwa kwenye hizi tafrija za kifahari ambazo watu wanaalikwa wachache. Nilifika mapema kabla ya tafrija na ilibidi nitafute mahali oa kutulia kwanza. Rafiki yangu alinialika kwake, alikuwa anasoma chuo cha TUM lakini alijitoa uhai. Katika chumba chake tulikuwa mimi na yeye na marafiki wa shuleni wawili, wenzetu wawili walikuja na wasichana wao. Watu sita ndani ya chumba hicho kimoja…” Chira alisimulia.
“Wote tulijivinjari kwa vinywaji hapa na pale, na mambo yakaenda mrama… kwa njia yenye nahisi nilichukuliwa faida kwa hali yangu. Kwa namna nyingine naweza nikasema nilibakwa. Na niliripoti kisa hicho niko na ushahidi wa kila kitu, nilirudi hadi chuoni Kabarak nikaripiti nikapewa PrEP… sikupewa maelezo kamili jinsi ya kutumia dawa hizo, nilikuwa natumia mara moja moja kwa kurukisha siku…” alisema.
Chira aliweka wazi kwamba katika mchakato ule wa kulewa, alichanganyikiwa na baadae ndio aligundua kwamba alilawitiwa na mwanamume.
“Nilipogundua nilikasirika na nilitoka hapo. Lakini walijuta kuhusu jinsi nitakavyokuwa katika hali yangu ya akili. Nilienda moja kwa moja na kupanda basi kurudi Nairobi.”
“Na hiyo hali iliendelea, unajua ni tembe 30 kwa hiyo mimi nilifikiria niko sawa baada ya kuzimaliza. Rafiki yangu akanialika baada ya miezi 3. Alikuwa kama ananipeleka chakula cha mchana lakini alikuwa na njama ya kunipeleka VCT. Nesi aliniita na kuniuliza kama nimewahi pimwa, akanipa ushauri na nikakunali kupimwa. Baadae nikapatikana niko na virusi. Ni kweli mimi ninaishi na virusi vya UKIMWI,” Chira alisema.