logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hakuna Mwanasiasa atakayekufa kwa ajili yako - Bahati awaonya waandamanaji

Msanii Kevin Bahati anawashauri Wakenya kutoruhusu siasa kuwagawanya.

image
na Davis Ojiambo

Burudani13 July 2023 - 08:00

Muhtasari


  • β€’ Bahati alisema, "Ndiyo sote tuna haki ya kujieleza lakini tusitumie fursa hiyo kupigana sisi kwa sisi, tusiitumie kumwaga damu, tusiitumie kuharibu mali ya masikini mwenzako kwa jina la Maandamano."
  • β€’ Aliongeza kuwa Rwanda ilipoteza Zaidi ya Watu Milioni 1 katika Siku zisizozidi mia moja kwa sababu ya Ukabila na Uchochezi wa Kisiasa.
Kevin Bahati anawashauri Wakenya kutoruhusu siasa kuwagawanya.

Msanii Kevin Bahati anawashauri Wakenya kutoruhusu siasa kuwagawanya kwani, hakuna mwanasiasa hata mmoja anayeweza kufa kwa ajili ya mwananchi hivyo basi anawashauri wananchi kutokubali kufa kwa ajili yao.

Alisema kuwa kutokana na kutazama habari kwenye maandamano alijihisi kusema kuwa iwapo vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya wananchi vikianza siku hiyo basi, Wanasiasa watachukua ndege ya kwanza na kukimbilia majuu.

"HAKUNA MWANASIASA MMOJA anayeweza kufa kwa ajili yako hivyo hupaswi kufa kwa ajili yao! Na Vita vya wenyewe kwa wenyewe Vikianza Leo Kenya Wanasiasa hawa Wataabiri Ndege ya Kwanza Wakimbilie Majuu... Huyo Mama Mboga unayemuibia ndio utakopa Sukuma Kwake Economy ikiumana," aliandika msanii huyo.

Msanii huyo aliendelea kwa kuelezea wananchi kuwa wajifunze kutoka kwa yale yaliyowapata wakati wa vurugu baada ya Uchunguzi wa 2007.

"Ndiyo sote tuna haki ya kujieleza lakini tusitumie fursa hiyo kupigana sisi kwa sisi, tusiitumie kumwaga damu, tusiitumie. kuharibu mali ya masikini mwenzako kwa jina la Maandamano," alisema kwa huzuni.

BAHATI on Instagram: "JUST FROM WATCHING THE NEWS ON MAANDAMANO and I Felt Like Saying Something... Before Reading this I would request you to take a Second and Watch this Short Video that I had Kept to Myself when I visited The Rwanda Genocide Memorial Rwanda πŸ‡·πŸ‡Ό Very Heart Breaking indeed πŸ’” It was Like a Bad Dream ; Rwanda Lost Over 1 Million People in less than a hundred Days Just Because of Tribalism and Political Incitement 😭 This was one of my hardest Moments in Rwanda, visiting the mass graves and listening to the Stories of how Blood was shed and Property Destroyed! Dear My Country People of Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ it all begins like this... We were loosing it in the year 2007 but God had Mercy on us; Let's learn from Our Neighbours Rwanda and especially what happened to us during the post Election Violence in 2007. Yes we all have a right to express ourselves but let's not use that opportunity to fight one another, let's not use it to shed blood, let's not destroy your fellow poor man's property in the name of Maandamano. I might not have succeeded as a Politician but I will tell you some plain Truth... NO SINGLE POLITICIAN can die for you so you should not die for any! And if Civil War Starts Today in Kenya this Politians will Take the First Flight Wakimbilie Majuu... The Mama Mboga you're stealing from ndio utakopa Sukuma Kwake Economy ikiumana. I Pray for strength to all Families who have lost their Loved ones Today and to my Fellow Youths being Used in this Protests; May God Protect You as you try to do it in a Peaceful way according to the Law without Destroying your Neighbours Property πŸ™ We are The Leaders of Tomorrow... so if We Loose our Youths To Gun shots Today Clearly there's No Tomorrow! May Peace and Unity Prevail in Jesus Name πŸ™ I LOVE YOU MY MOTHER LAND KENYA πŸ‡°πŸ‡ͺ"

Bahati alisema kuwa kutembelea makaburi ya halaiki na kusikiliza Hadithi za jinsi Damu ilivyomwagika na Mali Kuharibiwa ni moja ya Nyakati zake ngumu sana nchini Rwanda.

Aliongeza kuwa Rwanda ilipoteza Zaidi ya Watu Milioni 1 katika Siku zisizozidi mia moja kwa sababu ya Ukabila na Uchochezi wa Kisiasa.

"Naziombea Nguvu Familia zote zilizopoteza Wapendwa wao Leo na Vijana Wenzangu Wanaotumika katika Maandamano haya; Mungu Akulinde unapojaribu kuifanya kwa njia ya Amani kwa mujibu wa Sheria bila Kuharibu Mali ya Jirani πŸ™.

Sisi ni Viongozi wa Kesho... kwa hivyo tukiwapiga vijana wetu kwa risasi za bunduki Leo Ni wazi hakuna Kesho! Amani na Umoja viwepo kwa Jina la Yesu πŸ™ NAKUPENDA MAMA YANGU NCHI KENYA πŸ‡°πŸ‡ͺ," aliandika msanii huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved