logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati amlalamikia mkewe Diana Marua kwa kutomnyoa sehemu za siri

Katika utetezi wake, Diana Marua alidokeza kuwa mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili hapendi amnyoe.

image
na Samuel Maina

Burudani23 July 2023 - 09:44

Muhtasari


  • •Bahati alikiri kuwa na mkewe Diana amesaidia sana kuboresha usafi wake kwa mfano kuhusu suala la kubadilisha nguo za ndani mara kwa mara.
  • •Katika utetezi wake, Diana Marua alidokeza kuwa mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili hapendi amnyoe.

Wanandoa mashuhuri Diana Marua na mwimbaji Kelvin Bahati hivi majuzi walishiriki video ya mazungumzo ya wazi kuhusu baadhi ya masuala yao ya kibinafsi.

Katika video iliyoshirikiwa kwenye YouTube, wanandoa hao walijadili jinsi maisha ya usafi ya Bahati yamebadilika tangu rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 alipokuja katika maisha yake.

Bahati alikiri kuwa na mkewe Diana amesaidia sana kuboresha usafi wake kwa mfano kuhusu suala la kubadilisha nguo za ndani mara kwa mara.

“Awali sikuwa nabadilisha boxer, ningevaa moja mara tatu kwa wiki. Saa hii navaa tofauti siku tano kwa sababu nabadilisha,” Bahati alisema.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pia alikiri kwamba katika siku za nyuma hakuwa akinyoa makwapa na nywele za sehemu zake za siri lakini Diana alipokuja amekuwa akimnyoa.

Hata hivyo, alilalamika kuwa mama huyo wa watoto wake watatu amemnyoa mara mbili pekee katika miaka saba ambayo wamekuwa pamoja.

“Inakuwaje tumekuwa kwa ndoa kwa miaka saba na umeninyoa tu mara mbili?" Bahati alimlalamikia mkewe.

Katika utetezi wake, Diana Marua alidokeza kuwa mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili hapendi amnyoe.

“Wewe hutakangi. Kuna siku nilikwambia kuja nikunyoe kwa bafu, uliniambia sio wakati mzuri mpenzi, ukaniambia nitakunyoa tukifika Dubai,” Diana alieleza.

Pia alifichua kuwa mara nyingi anaponuia kumnyoa Bahati, baba huyo wa watoto wake watatu kwa kawaida huwa analalamika kwamba atajihisi kuwashwa.

Siku ingine nikakwambia ukuje nikunyoe, ukakataa ukaniambia utaanza kuskia kujikuna,” alisema.

Aliongeza, “Mara ya mwisho nilimwambia Baha twende nikunyoe saa hii, aki ilikuwa ni kama unaweza zishuka nywele zako na uweke beads.”

Rapa huyo mrembo hata hivyo alimuahidi mumewe kuwa atamnyoa na kupaka eneo hilo dawa ambayo ingezuia kuwashwa. Hii ilikuwa baada ya baba huyo wa watoto wanne kufichua kuwa kwa sasa nywele  zake zimekua kubwa sana.

Diana Marua alijisia kwamba amekuwa na athari chanya katika maisha ya mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na akadokeza kuwa maisha yake yangekuwa mabaya sana bila yeye.

"Maisha yako bila mimi ni duni. Haki mimi nakuhurumianga,” alisema.

Bahati na Diana wamekuwa pamoja kwa takriban miaka saba na tayari wamejaliwa kupata watoto watatu pamoja. Pia wanalea mvulana wa miaka 13 ambaye Bahati alimchukua kutoka chumba cha watoto yatima

Ni miongoni mwa wanandoa waliosherehekewa zaidi na pia kukosolewa zaidi, sababu kuu ikiwa kuwa Diana ana umri mkubwa kuliko mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili. Hata hivyo, wote wawili wanaonekana sawa na hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved