Mchekeshaji mashuhuri Eric Omondi amepuuzilia mbali madai ya kuchafua maji wakati wa hafla ya kufichua jinsia ya mtoto wake ambaye hajazaliwa.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Eric na mpenzi wake Lynne walifichua jinsia ya mtoto wanayemtarajia kwa njia ya kipekee ambapo maji ya mto yalibadilishwa rangi na kuwa waridi kutangaza kuwa wanatarajia msichana. Hatua hiyo hata hivyo ilivutia ukosoaji mwingi kutoka kwa wanamitandao wa Kenya ambao waliwashutumu kwa uchafuzi wa mazingira
Katika mahojiano na kituo moja cha redio cha humu nchini, mchekeshaji huyo hata hivyo alifichua kuwa chakula cha samaki kilichowekwa rangi asilia ya vyakula kilitumika kubadilisha rangi ya maji ya mto.
“Hatujachafua mazingira. Pale kwenye maji kuna vitu ambazo unaweza kutumia ambazo ni kama chakula cha samaki, kuna organic colors. Sio rangi kama ya kupaka kwenye ukuta,” Eric Omondi alieleza.
Eric alisema waliomba kibali kutoka kwa maafisa wa maji kabla ya kununua chakula cha samaki na rangi ya asili ya chakula katika eneo la Industrial Area na kisha kuweka kwenye maji hayo.
“Kile ni chakula cha samaki, tumechezea tu. Ni chakula cha samaki tumeweka food color. Tumetulia, tumechukua muda, tumefanya utafiti, tumeuliza hadi tukakuja na kuja,” alisema mchekeshaji huyo.
Alieleza kuwa bidhaa zilizotumika hazikuwa na kemikali hatari kama ilivyodaiwa awali na watumizi wa mitandao.
Wikendi, Eric Omondi na mpenziwe Lynne walitangaza wanatarajia msichana kwa kutumia maji ya maporomoko ambayo yalibadilishwa rangi kuwa waridi.
Marafiki wa karibu wa wapenzi hao pia walihudhuria karamu hiyo ya kufana iliyoandaliwa mjini Thika.
“Ni Mtoto wa Kike,” alisema Omondi.
Ingawa baadhi ya mashabiki wa wapenzi hao waliwasifu kwa uvumbuzi wao wa jinsia, wengine wao waliwakosoa kwa kuharibu mazingira.
Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao:-
Miss fifiture: This behavior should be called out!!!! How selfish can humanity be ruining freshwater and all the lovely creatures living inside it
Africatoficial: This is so gross man... Kenyan rivers are already polluted enough without people doing it for fun. It's going to kill anything that lives in that river and poison someone downstream .
Itsyougene: Destroying the natural ecosystem is now becoming a celebrated trend... SHOCKING
Pridenkenya: Water pollution 😒
Ogkagz: What was that poured in the river? Ain't that water pollution, though?
Whook: A wrong is a wrong and just cause majority do it don’t make it right. But again maybe what they used is not toxic
Awuor Atieno: even the ones who do with aeroplane still cause air pollution,bana please allow people to rejoice in thier moment of glory
Victoria Shiko: oh dear! Here is the death of our planet