Machafuko katika mzunguko wa maisha ya msanii namba moja wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido hayaonekana kufikia mwisho muda wowote kwani kila yanayoonekana kuchukua likizo, mengine yanachibuka – mabaya kwa mazuri.
Athari kubwa ya matukio hayo inakisiwa kupiga pale pale kwenye mshono wa mkewe, Chioma, ambaye amepitia mambo mengi kutoka mwishoni mwa mwaka jana mwanawe alipofariki hadi mwaka huu mumewe alipotuhumiwa na wanawake kadhaa kuwa na watoto na yeye, wengine wakitangaza kuwa na mimba zake.
Kulingana na blogu ya Instablog9ja, Baby mama wake mwenye utata kutoka Marekani, Anita Brown alitangaza saa chache kwamba Davido na mchepuko wake Amanda wamemkaribisha mwanao wa pili, mrembo huyo alikwenda mbele na kufichua picha za kitoto hicho kichanga.
Kulingana na blogu maarufu ya Instagram, Instablog9ja, picha inayodaiwa kuwa ya mtoto wa pili wa Davido na babymama Amanda akiwa na binti yao wa pili pamoja imezua hisia mtandaoni.
Kumbuka kwamba mnamo Mei 2023, tuliliripoti kuwa Amanda alikuwa mjamzito na alikuwa tayari kumkaribisha mtoto mwingine wa nyota huyo wa Afrobeat.
Hata hivyo, blogu hiyo iliripoti baadae kwamba Amanda mwenyewe alikanusha madai ya kupata mtoto wa pili na Davido na kumtaka Anita Brown kukoma kueneza uvumi usio na tija.
“Nimeamka na habari za kushangaza, yaani siwzi hata pakia picha ya mtoto wa rafiki yangu bila nyinyi watu kuongea upuuzi,” babymama wa pili wa Davido, Amanda, anamwambia anayedaiwa kuwa ni mchepuke mwenza Anita, huku akikana habari za mtoto wa pili.
“Nyinyi watu ni wajinga niacheni tafadhali. Huwa sizungumzii upuuzi lakini acha jina langu nje ya midomo yenu kuhusu haya madai na uvumi wa uongo. Mawazo yenu yananitisha na ni wakati mwende mtafute kitu kingine cha kufanya kuliko kufuatilia watu mitandaoni, kwani hamchoki?” aliongeza.