logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee afurahi kuona bintiye akishiriki mchezo hatari na mchumba wake - Video

"Tazama huyu mkwe wangu amemchukua binti yangu pia" - Akothee.

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 July 2023 - 07:36

Muhtasari


  • β€’ Msanii huyo alipakia klipu ya mchezo mmoja wa kuhatarisha ambao binti yake mdogo Fancy Makadia alikuwa anashiriki na mpenzi wake.
akothee,

Ni furaha ya kila mama kumuona mwanawe akiwa anatabasamu; kila mama anataka kuona tabasamu katika uso wa binti yake haswa anapompata mpenzi.

Akothee ni mama wa aina hiyo ambaye hachoki kufurahia maisha ya mabinti zake wakubwa ambao sasa wana uhuru wa kutoka kimapenzi na wanaowapenda.

Msanii huyo alipakia klipu ya mchezo mmoja wa kuhatarisha ambao binti yake mdogo Fancy Makadia alikuwa anashiriki na mpenzi wake.

Makadia na mpenzi wake walionekana kuwa katika chombo kimoja cha kielektronini wakiwa wamelala juu ya chombo hicho kiocho kama jahazi huku kila mmoja ameshikilia kwa nguvu wakitelezeshwa katika kile kilionekana kama ni theluji kwa kasi ya ajabu.

Akothee aliwapa mashabiki wake kionjo cha mchezo huo na kufurahia jinsi binti yake alikuwa anapunja maisha na mpenzi wake, lakini pia akaonesha wasiwasi wake kama mama kuhusu mchezo huo ulionekana kuwa wa kuhatarisha maisha.

Mama huyo wa watoto watano alimuusia Makadia kuwa makini katika mchezo wake na mpenziwe, haswa baada ya klipu hiyo kumalizia ikimuonesha akianguka kutoka kwa chombo hicho na kugaragara kwa kasi kweney sakafu ya theluji.

“Kuzaa ni kama kuruhusu moyo wako kuondoka kwenye ubavu wako. Tazama huyu mkwe wangu amemchukua binti yangu pia. Oyaaa, tafadhali abeg, huyo ni mtoto wangu wa mwisho wa kuzaliwa wa Kiafrika nichungie tafadhali Mhandisi @fancy_makadia mchezo gani huu πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€” Sasa ukivunjika shingo utasema nini? Ati mapenzi yana run dunia, Dunia gani?” Akothee alisema.

Mashabiki wa Akothee walioona mchezo huo hatari walitoa maoni tofauti, wengine wakisema kuwa angekuwa ni yeye na mumewe Omoshi wala asingejali kuhusu usalama wa shingo.

Wengine walisema kuwa wasiwasi ndio akili, wakisema kuwa hawawezi ruhusu wanao kushiriki katika michezo kama hiyo.

β€œMama ni Mama moyo wangu uliruka hii hapana” mama mmoja alisema.

β€œπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Inge kua ni ww na omoshi uwenzi sema mambo na shingoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚β€ mwingine alimtania.

β€œπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hii inatisha ingawa πŸ˜‚πŸ˜‚β€ momo Nanjumba alisema.

Wewe ungeruhusu mwanao kushiriki katika mchezo kama huu?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved