logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nimetimuliwa chuoni kufuatia mitikasi yangu mitandaoni - Brian Chira

Brian Chira amefichua kuwa ametimuliwa kutoka chuo kikuu cha Kabarak.

image
na Davis Ojiambo

Burudani01 August 2023 - 10:08

Muhtasari


  • • Chira alieleza kuwa chanzo kuu ni kuwa shule hiyo yenye misingi ya kikanisa ilihisi matendo yake mitandaoni ilienda kinyume na hili.
  • • Siku ya Jumatatu, Brian Chira alifikishwa mahakama ya Kibera baada ya kukamatwa siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa mitandaoni.
Brian Chira

TikToker maarufu Brian Chira amefichua kuwa amedai kufukuzwa kutoka chuo kikuu cha Kabarak kwa sababu makala yake kwenye mitandaoni iliyokuwa ikienda kinyume na kanuni za Chuo hicho.

Chira akizungumza kwenye mahojiano na Andrew Kibe baada ya kuachiliwa na mahakama ya Kibera kwa dhamana ya shilingi 50,000, alieleza kuwa chanzo kuu ni kuwa shule hiyo yenye misingi ya kikanisa ilihisi matendo yake mitandaoni ilienda kinyume na hili.

"Nimetimuliwa chuoni kwa sababu kulingana na chuo kikuu cha Kabarak ambayo motto yake ni elimu kwa misingi ya kikanisa na kwa hivyo walihisi kuwa vitendo vyangu mitandaoni haikuendanisha na motto yao."

Chira aliongeza kuwa alikamatwa na polisi alipokuwa chuoni baada ya kushtakiwa na muunda maudhui mwenza Azziad Nasenya kwa madai ya kumchfulia jina.

Siku ya Jumatatu, Brian Chira alifikishwa mahakama ya Kibera baada ya kukamatwa siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa mitandaoni na kuweza kutumia akaunti yake ya TikTok na kumtukana Azziad.

Kulingana na Getrude Kibare, wakili wa Azziad, live ya Chira kwenye mtandao wa Tiktok ilikuwa na matamshi ya kuudhi yaliyomlenga Azziad, yakitumia lugha mbaya na ya kudhalilisha.

Wakati huo huo, Chira alifichua bila kujali maelezo ya kibinafsi ya Azziad mtandaoni, na kumfanya apokee simu nyingi ambazo zinazomsumbua kutoka kwa watu asiowajua. jambo ambalo lilimsababishia dhiki kubwa.

Waunda maudhui ikiwa ni pamoja na Eric Omondi  na Oga Obinna walijitokeza na kumkashifu Chira kwa matusi aliyomtupia Azziad wengi wao wakisema ilikuwa muda mwafaka kwa watu wanatumia umaarufu wao kuwanyanyasa wenzao mitandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved