Rapa namba moja wa Kenya Khaligraph Jones ametamba kwamba anajiamini na kujijua kuwa hakuna msanii mwingine wa rap anayeweza kutokea na kumpiku katika kurap.
Akizungumza na Obinna, Khaligraph alidai kwamba yeye ndiye namba moja katika Hip Hop ya Kenya wala watu wasijaribu kumlinganisha na wasanii wengine.
Khaligraph alisema kwamab marapa wengine kama mshindani wake wa muda mrefu Ooctopizzo na King Kaka wala hawamfikii hata kidogo katika kutema madini ya mistari.
Khaligraph alisema kuwa wawili hao wanaweza tu kumshinda katika fasheni ya mavazi lakini ikifika ni kwenye kushika kipaza sauti wasahau kabisa kwani atawaonesha kivumbi.
“Hao wananiweza katika kurap kweli? Tuongee tu ukweli, wananiweza? Kaka kurap? Labda katika kitu kingine kama kuvaa nguo wanaweza kunishinda lakini kwa kurap hawaniwezi. Labda unitajie mtu mwingine,” Khaligraph alisema.
Hata hivyo, Khaligraph alikubali kwamba msanii Nyashinski ndio pekee anayeweza kumpa ushindani kidogo tu lakini akasisitiza badi hawezi mshinda.
“Nyash ni mnoma lakini bado hawezi nishinda. Lakini pia nisingependa kujiweka kwenye ligi yake kwa sababu Nyashinski ni msanii ambaye nilifuata nyayo zake. Ni jamaa ambaye nilikuwa naona nikiwa mdogo lakini sasa unajua tuko kwenye tasnia moja kizazi hiki lakini niko na heshima kubwa sana kwake hata naweza nikaimba wimbo wake mzima,” Khaligraph alisema akionjesha mistari ya wimbo wa zamani wa Nyashinski.
Khaligraaph alisema kuwa utakuwa mtu mjinga kama huwezi kumheshimu Nyashinski kwani amekuwepo kwa muda mrefu.
Khaligraph alisema kuwa wasanii wa kisasa ambao anaweza kuwatambua kidogo katika kurap ni kama Scar Mkadinali kutoka kundi la Wakadinali, Breeder, Trio.
“Lakini unajua mimi nitakuwa na furaha sana nikiona watu wakiinganisha Trio Mio na King Kaka na kusema Trio ni mnoma, nitafurahi,” Trio Mio alisema.