logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Acheni kelele chui kalalia chakula chake - Fahyma kuhusu Rayvanny kulalia makalio yake

"Acha kelele, chui kalala," aliandika.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 August 2023 - 08:25

Muhtasari


  • • Mwishoni mwa wiki jana, tuliripoti kwamba ilikuwa inakisiwa kuwa na mporomoko katika penzi lao.
  • • Wawili hao walionekana kuacha kufuatana Instagram .
Rayvanny na Fahyvanny.

Agosti 22 amabyo ilikuwa Jumanne, ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya msanii mmiliki wa lebo ya Next Level, Rayvanny.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mpenzi wake Fahyvanny alimsherehekea kwa ujumbe wenye makopakopa mengi akimuita kama mume wake na kuahidi kuganda kwenye ubavu wake katika miaka mingi ijayo.

Wawili hao walishiriki mfululizo wa picha zao za pamoja wakifurahia siku kubwa kwa bosi huyo wa NLM na mojaya picha ambayo ilinasa macho ya watu ni ile Rayvanny akiwa amemalia makalio ya mpenzi wake.

Hata hivyo, Fahyma aliwazima akiwaambia kukoma tantarira nyingi kwani Rayvanny hajakosea.

"Acha kelele, chui kalala," aliandika.

Katika ile hali ya kutaniana, Fahyvanny alimtaka Rayvanny kuwa muelewa katika ndoa ili kuepusha malumbano ya mara kwa mara, akikiri kwamba ni kweli ana kidomo domo sana lakini kubwa mwisho wa siku ni kumuelewa na kumsamehe.

Namuomba MUNGU atujaalie na atutimizie kila hitaji la mioyo yetu🙏. Nakuombea mafanikio mengi ktk kazi zako mumewangu, Nakupenda, nakuthamini na kuheshimu pia. Tusameheane pindi tunapokosana Binafsi naomba tu univumilie maana nina mdomo sana,” Fahyvanny alisema.

Alikwenda mbele na kumtahadharisha Rayvanny kwamba kitu ambacho nacho hawezi kuacha kabisa ni kuchakura simu yake ili kuona vipusa wanaommezea baba mtoto wake mate kwenye faragha za mitandao ya kijamii.

“Na kingine mume wangu simu yako kushika siachi hilo ulijue. Nakupenda sana sana kuliko chochote hapa duniani️” Fahyvanny aliongeza.

Mwishoni mwa wiki jana, tuliripoti kwamba ilikuwa inakisiwa kuwa na mporomoko katika penzi lao baada ya kubaini kwamba walikuwa wameacha kufuatana katika mitandao ya kijamii.

Lakini kama inavyoonekana ilikuwa ni kama kuwachezea shere mashabiki wao kwani kwa kile ambacho kinaonekana wawili hao wamezama katika kina kirefu sana cha huba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved