Amber Ray akejeliwa baada ya Vera kuonyesha kitanda cha bintiye chenye thamani ya nusu milioni

Baadhi ya mashabiki walimpongeza huku wengine wao wakimshutumu kwa kudanganya kuhusu hilo.

Muhtasari

•Jumatatu, Vera Sidika alionyesha picha za chumba cha kulala kizuri cha binti yake Asia Brown chenye samani za kifahari.

•Vera alieleza kuwa jumla ya gharama ya kitanda hicho ni kubwa kwani mbali na kuwa na ubora wa hali ya juu, pia ililazimika kubebewa hadi Kenya kwa ndege.

alidhihakiwa baada ya Vera kuonyesha kitanda cha bintiye chenye thamani ya nusu milioni
Amber Ray alidhihakiwa baada ya Vera kuonyesha kitanda cha bintiye chenye thamani ya nusu milioni
Image: INSTAGRAM

Siku ya Jumatatu, mwanasosholaiti wa Kenya Vera Sidika alionyesha picha za chumba cha kulala kizuri cha binti yake Asia Brown chenye samani za kifahari.

Moja ya samani zilizonaswa kwenye picha hizo alizochapisha kwenye Instagram ni kitanda cha Asia ambacho alidai kina thamani ya takriban shilingi laki tatu.

Mama huyo wa watoto wawili alidai kuwa aliingiza kitanda hicho kidogo cha kifahari kutoka Uingereza kwa gharama ya takriban shilingi laki mbili na hivyo kusukuma matumizi ya samani hiyo hadi takriban shilingi nusu milioni.

“Hiki kitanda cha mtoto cha 500k kutoka Uingereza kinastahili kabisa!!! Cha kifahari na maalum kwa nyumba ya binti ya mfalme,” Vera Sidika alisema chini ya picha alizochapisha.

Wanamitandao wengi walioona chapisho hilo walionekana kushangazwa na bei isiyo ya kawaida iliyodaiwa kuwa ya kitanda hicho cha msichana huyo wa miaka miwili.

Vera alieleza kuwa jumla ya gharama ya kitanda hicho ni kubwa kwani mbali na kuwa na ubora wa hali ya juu, pia ililazimika kubebewa hadi Kenya kwa ndege.

"Nyinyi nyote ni wa kushangaza sana katika maoni.. Kitanda: pauni 1770, usafirishaji wa pauni 1226, jumla ya pauni 3000, hiyo ni Sh584,000. Bila shaka kitanda hakiwezi kuota mbawa na kuruka chenyewe hadi Kenya,” alisema.

Kundi la mashabiki wake walimpongeza mke huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo kwa kufanikiwa kununua samani hiyo ya bei ghali huku baadhi yao wakimshutumu kwa kudanganya kuhusu hilo.

Wengine ambao walitoa maoni yao katika sehemu za maoni walionekana kutupa vijembe kwa mmoja wa mahasidi wakubwa wa Vera Sidika, Amber Ray ambaye hivi majuzi alimshutumu kwa kufeki maisha yake ya kifahari.

Tazama baadhi ya maoni hapa chini;-

joe_maureen:Vera is the Tajiri not others ati bibi ya tajiri😂😂

lindatuju:Uzuri Otis de furniture anaweza make hii bed na 35k..

panelope_pea: at least vera ni tajiri by herself,si bibi ya tajiri 😂

r053b:Enyewe sisi wengine tunawasindikiza tu katika hii safari 😁 sisi ni obwolo 😂

saumuchangawa: Sema Vera unajua mpaka unakera alafu mwengine anaringa na pesa za bwana nkt😂😂

maryliya84: Bibi ya tajiri atapost after 10 minutes