"Naskia kuongeza mwingine!" Nadia Mukami afichua kwa nini ana hamu ya kupata mtoto wa pili

Nadia na Arrow Bwoy walimkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza ,Haseeb Kai mwezi Machi mwaka jana.

Muhtasari

•Nadia alifichua kuwa Kai ameanza kukosa raha nyumbani, jambo ambalo limempa mawazo ya kupata mtoto mwingine.

•Hivi majuzi, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 26 alikiri kwamba ametiwa hofu sana na maendeleo ya haraka ya mwanawe.

amesema mtoto wake Haseeb Kai ameanza kuboeka nyumbani
Nadia Mukami amesema mtoto wake Haseeb Kai ameanza kuboeka nyumbani
Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAMI

Malkia wa muziki wa Kenya Nadia Mukami amefunguka kuhusu hamu yake ya kupata mtoto mwingine na mchumba wake Arrow Bwoy, takriban mwaka mmoja na nusu tu baada ya kubarikiwa na mtoto wao wa kwanza Haseeb Kai.

Katika chapisho la siku ya Jumamosi, Nadia alishiriki picha nzuri zinazomuonyesha akiwa na mwanawe Kai ambaye amekuwa mkubwa sana huku wote wakionyesha tabasamu zuri kwenye nyuso zao.

Katika sehemu ya maelezo,alifichua kuwa hata hivyo mvulana huyo wa umri wa mwaka mmoja ameanza kukosa raha nyumbani, jambo ambalo limempa mawazo ya kupata mtoto mwingine.

“Naskia kuongeza mwingine. Kai ameanza kuboeka. Huu upendo @Haseebkai,” Nadia aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Hivi majuzi, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 26 alikiri kwamba ametiwa hofu sana na maendeleo ya haraka ya mwanawe.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram,  alichapisha picha za Kai na akabainisha kuwa mvulana huyo  anakua zaidi kila siku.

Wakati huo, Nadia alifichua kuwa kwa vile mwanawe anakua, anahofia kwamba hivi karibuni anaweza kuanza kumtaka abishe mlango wake kwanza kabla ya kuingia au hata kumtaka akome kumbusu wakati wowote akidai kuwa ni aibu.

"Ninaogopa kwamba anakua na hivi karibuni atasema mama tafadhali bisha au hata kusema mama achana na chum (busu) unaniaibisha," Nadia Mukami alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja alibainisha kwamba kusikia amri kama hizo kutoka kwa mwanawe kunaweza kumfanya azidiwe na hisia hadi kulia.

Wakati huo huo, pia alidokeza kuhusu uhusiano wa karibu sana na wenye nguvu kati yake na Kai.

“Nimezidiwa na upendo!! Ikiwa niliwahi kumhukumu Kijana wa mama tafadhali. Nisamehe! Sasa najua vizuri zaidi!!,” alisema.

Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bwoy walimkaribisha  mtoto wao Haseeb Kai duniani mwezi Machi mwaka jana.

"24.03.2022 tumepokea zawadi nzuri zaidi Haseeb Kai. Karibu kwenye ulimwengu wetu," Arrow Bwoy alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hapo awali wanandoa hao walikuwa wamepoteza ujauzito wa ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza.