Fahamu hasara kubwa ambayo Diamond alipata Wikendi

Meneja alidhibitsha walipata hasara ya milioni 93 za tanzania, ambazo ni sawa na takriban milioni 5.4 za kenya.

Muhtasari

•Diamond alikuwa amealika makumi ya wasanii kucheza muziki mbalimbali wakati wa shoo hiyo iliyopangwa na  kikundi cha wasafi.

•Mkubwa Fella alisema , ‘’tulimweka Mungu mbele maanake tulikuwa tunaonyesha upendo wetu kwa mashabiki.’’

Image: Instagram

Msanii tajika wa nyimbo za bongo  Diamond platinumz alikumbwa na hasara kubwa  wakati wa tamasha la muziki liliofanyika Mtwara nchini Tanzania.

Msanii huyo alikuwa amealika makumi ya wasanii kucheza muziki mbalimbali wakati wa shoo hiyo iliyopangwa na  kikundi cha wasafi.

Chini ya muda wa dakika thelathini baada ya Diamond platinumz kuingia jukwaani, kulitokea hitilafu ya nguvu za umeme, jambo ambalo lilimwacha msanii huyo kinywa wazi ashindwe cha kufanya, ila alilazimika kuwatuliza mashabiki wake na kuwaahidi tamasha la bure kesho yake.

Mmoja wa menega wa msanii huyo,bwana Mkubwa Fella, alidhibitsha  kukadiria hasara ya milioni 93 za tanzania, ambazo ni sawa na takriban milioni 5.4 pesa taslimu za kenya.

‘’Hasara ni kubwa,kubwa zaidi ya hiyo kwa maana hatukuweza kuhesabu. Kwa sababu, kuna jukwaa,sauti, na uwanja vilevile,halikadhalika wasanii ikizingatiwa kwamba onyesho lilikua la bure, na lilifanywa kwa siku mbili’’ Alisema.

’Tulilazikima kulipa wasanii mara mbili.’’

Aliongeza kuwa, ‘’mwisho wa siku, mola ndiye Mpaji. Msanii alikua amecheza  nyimbo nne na hivyo hatukutosheleza mashabiki.’’

Aidha meneja huyo alisema , ‘’tulimweka Mungu mbele maanake tulikuwa tunaonyesha upendo wetu kwa mashabiki.’’

Akitangaza kuahirisha tamasha hiyo, msanii diamond alikua na haya ya kusema,

‘’MTWARA!!!!!!!MTWARA!!!!! kutokana na hitilafu ya umeme jana katika show yangu,leo kuanzia asubuhi mpaka saa 12jioni nina wasanii mbalimbali wa wasfi festivals tutakua tunaperform tena live katika uwanja wa NANWADA.’’