logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Brown Mauzo arudi sokoni kutafuta rafiki mzuri wa kulala na yeye

“Natafuta rafiki mzuri ambaye naweza nikalala na yeye,” Brown Mauzo alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 September 2023 - 09:12

Muhtasari


  • • Mauzo alivunja ukimya huo ikiwa ni wiki moja baada ya kukiri kwamba yeye na mama watoto wake wawili hawako pamoja tena.
  • • "Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu," alisema.
Brown Mauzo

Msanii kutoka ukanda wa Pwani, Brown Mauzo siku chache baada ya kudhibitisha kuachana na mwanasosholaiti Vera Sidika, ametangaza kurudi sokoni.

Mauzo kupitia Insta story yake aliandika ujumbe wa kuthibitisha hilo akisema kwamba yuko sokoni kumtafuta rafiki mzuri ambaye anaweza akalala na yeye pasi na taabu.

“Natafuta rafiki mzuri ambaye naweza nikalala na yeye,” Brown Mauzo alisema.

Mauzo alivunja ukimya huo ikiwa ni wiki moja baada ya kukiri kwamba yeye na mama watoto wake wawili hawako pamoja tena.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mauzo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

 

Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa Zaidi ya miaka mitatu ambapo katika kipindi hicho wakibarikiwa na watoto wawili, wa kike na wa kiume.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved