Kwa muda wa Zaidi ya miaka 15 kumekuwa na mjadala mkali mitandaoni baina ya wachanganuzi mbali mbali wa soka wakibishana na wakati mwingine kutofautiana vikali kuhusu ni nani mkali wa kusakata soka kati ya mchezaji nambari moja kutoka Ureno Christiano Ronaldo na mchezaji mwenzake vile vile nambari moja kutoka Argentina Lionel Messi.
Kutoka kwa wachezaji wa zamani, makocha na sasa hadi wasanii wa muziki tofauti wamekuwa wakiwekwa katika kikaango kuhusu kuchagua aliye bora kati ya wawili hao, pindi tu swali la ushabiki wa mpira wa kandanda linapojitokeza.
Safari hii ilikuwa ni msanii namba moja wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido ambaye alilazimika pia kutoa chaguo lake kuhusu ni mchezaji yupi bora kati ya hao wawili ambao wametawala soka kwa karibia miongo miwili sasa.
Davido, ambaye aligonga vichwa vya habari kutokana na uchezaji wake katika Tuzo za Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA) 2023, alimchagua Ronaldo kama mwanasoka bora zaidi wa wakati wote mbele ya Messi.
Davido alimuelezea nyota huyo wa Ureno kama mtu mwenye nidhamu kama yeye alipojitangaza kama 'kijana wa Ronaldo'.
Bosi huyo wa DMW pia alimtaja winga wa Arsenal Bukayo Saka kuwa mchezaji wake kijana anayempenda kwa sasa.
Kwa maneno yake:
"Cristiano kwangu, unajua, matokeo gani, nidhamu sana, sana. Mimi ni mtu mwenye nidhamu sana, unajua, na kuwa na aina hiyo ya mafanikio na kuwa na nidhamu wakati huo huo ni jambo ambalo nimekuwa nikivutiwa naye kila wakati. Nawapenda wote wawili. Lakini, mimi binafsi, mimi ni mvulana wa Ronaldo.”
Maneno haya yanakuja siku chache baada ya Ronaldo kuweka wazi kwamba japo yeye si shabiki wa Messi lakini wao wanaheshimiana huku wakisema kuwa shabiki wake hawafai kumchukia shabiki wa Messi kwani wawili hao walileta mbwembwe uwanjani kwa Zaidi ya miaka 15.
Tazama video hapa chini: