logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu kwa nini msaani Ney wa Mitego amefungiwa kufanya shoo Tanzania

Nay wa Mitego wa Tanzania amefungIwa kufanya matamasha nchini humo kutokana na wimbo wake wa ‘Amkeni’.

image
na Samuel Maina

Burudani08 September 2023 - 04:20

Muhtasari


  • •Nay wa Mitego wa Tanzania amefungIwa kufanya matamasha nchini humo kutokana na wimbo wake wa ‘Amkeni’.
Msaani Ney wa Mitego afungiwa kufanya maonesho Tanzania

Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama ‘Nay wa Mitego’ wa Tanzania amefungIwa kufanya matamasha nchini humo kutokana na wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Ingawa hakusema amefungiwa kufanya matamasha kwa muda gani, Wakili wa Msanii huyo, Jebra Kambole ameithibitishia BBC kwamba Msanii huyo anatuhumiwa na vyombo viwili.

‘Moja kuna kinachoendelea BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania) , na kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, BASATA wana malalamiko wakisema wimbo alioutunga (Amkeni) unaonekana una maneno ya uchochezi, lakini sio hilo tu, wameufungia wimbo wenyewe na wamemkataza kufanya matamasha kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’, alisema Kambole.

Kuhusu Polisi Jebra aliongeza; ‘Kinachoendelea Polisi ni kwamba jana aliitwa akipewa tuhuma kuhusiana na wimbo huo huo (Amkeni), ambao unaonekana una mashairi ambayo wao wanadhani kwamba ni ya uchochezi, tulitoa maelezo ya kwanini tunaona kwamba sio ya uchochezi na tukawaachia Polisi wafanye kazi yao’.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved