Mwigizaji wa Tanzania Elizabeth Michael, anayetambulika kama Lulu amekutana na mama wa mpenzi wake wa zamani Kanumba.
Steven kanumba alikuwa mwigizaji kipenzi wa filamu za Bongo ambaye alishabikiwa na watu wengi. Alifariki dunia kwa madai ya kuzozana na mpenzi wake wa wakati huo Elizabeth Michael.
Elizabeth alifungwa jela kwa kuua bila kukusudia na kuwekwa gerezani kwa miaka miwili.
Kwa miaka mingi sasa, mamake Kanumba amekuwa akimulaumu kwa kifo cha mwanawe. Wawili hao hawajawahi kuonana macho kwa macho na kwa mara ya kwanza waligonga vichwa vya habari walipopatana kwa mara ya kwanza na kushirikishana wakati wa hisia pamoja.
Elizabeth alipoonana na mama mkwe alimwambia;
"Ni muda mrefu hatujaonana, muda mrefu sana," Elizabeth alionyasha furaha kubwa.
Ajuza huyo aliye jawa na furaha ya kumwona mpenzi wa mwanawe, aalimjibu Elizabeth akisema;
"Tunamshukuru Mungu."
Elizabeth Michael alikuta na hatia ya kuua bila kukusudia na alihukumiwa kifungo cha miaka miwili mnamo mwezi Novemba mwaka wa 2017 baaada ya kifo cha mumewe Kanumba kilichotokea mwaka wa 2012.
Inasemekana Kanumba alifariki dunia baada ya kupata jeraha kichwani akiwa chumbani kwake baada ya kuzozana na mkewe Elizabeth.
Aidha Elizabeth alieleza kuwa alikua akijitetea dhidi ya mwigizaji marehemu, ambaye alimgonga kichwa baada ya kuteleza.
Elizabeth Michael, amewahi kupokea tuzo nyingi zaidi kutokana na uigizaji wake. Ikiwemo ni pamoja na, Tuzo ya Zanzibar International Films Festival, tuzo ya mwigizaji bora, Tuzo Africa Magic viewrs Choice za 2016 za filamu bora Afrika Mashariki,pamoja na zingine nyingi.
Kanumba alishabikiwa sana kwa uigizaji wake wa kupigiwa mfano. Kifo chake cha mwaka wa 2012, kiliwaacha wengi na uzuni kwani walipenda kufuatilia filamu zake. Kanumba aliaga dunia akiwa na mika 28 kabla ya kifo chake.