Kando na kusema Diana hawaolewi, tazama kauli zingine tata za mchungaji Ezekiel Odero

Mchungaji Ezekiel amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kusikika akiwaonya wanaume dhidi ya wanawake wanaoitwa Diana.

Muhtasari

•Wakati wa moja ya mahubiri yake, kiongozi huyo wa kanisa la Newlife Prayer Center alisikika akiwaonya wanaume dhidi ya kuoa wanawake wanaoitwa Diana.

•Ezekiel aliwahi kusema,"Ikiwa mke wako ana tattoo kwa shingo, kifua, miguu, mikono, mapaja, basi jiandae kushare na watu."

Mchungaji Ezekiel Odero.
Mchungaji Ezekiel Odero.
Image: MAKTABA

Mchungaji maarufu wa Kenya Ezekiel Odero amekuwa akivuma saa kadhaa zilizopita kufuatia kauli tata alizotoa kuhusu wanawake wanaoitwa Diana.

Wakati wa moja ya mahubiri yake, kiongozi huyo wa kanisa la Newlife Prayer Center alisikika akiwaonya wanaume dhidi ya kuoa wanawake wanaoitwa Diana.

Alisema kwamba kina Diana hawakukusudiwa kuolewa na ikiwa watajipata wameingia kwenye ndoa, basi wanadhibiti ndoa hiyo.

“Umeshawahi kuona Diana yeyote kwa ndoa? Hakuna hata mmoja hivi. Ukioa Diana uishi na yeye, yeye ndiye anakuongoza kama robot anakubeba hivi, utaishi na Diana, anakuwa mwanamume. Lakini wewe uwe mume, Diana anaenda. Hapo nimeongea ukweli,” Ezekiel anasikika akisema kwenye video inayosambaa.

Jambo la pili ambalo aliwashauri waumini wake ni kukoma kuwapa wanao jina  Diana akisema ni jina lenye historia isiyo nyooka.

“Usimpe mtoto wako jina Diana, sababu akiolewa, utamshare na watu, Diana anapendwa bila sababu hata kama hajui. Bila yeye kujua, mtu anamwambia nikikwangalia akili inachanganyikiwa, kwa sababu jina hilo linabeba roho mbaya,” Ezekiel alisema.

Matamshi ya mtumishi huyo wa Mungu mwenye makazi yake katika eneo la Pwani yamealika hisia mseto kutoka kwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Ezekiel kutoa kauli tata na kuzua mjadala mkubwa mitandaoni, tazama kauli zingine alizowahi kuzitoa siku za nyuma;-

i) Kina Diana hawaolewi, wakiolewa wanatawala ndoa.

ii) Usimuite mtoto wako Diana. Ukifanya hivyo, hatakuwa wako pekee. 

iii) Hakuna mwanamke mwenye rasta ako na bwana. Na kama ako bwana, basi ako njiani anaenda.

iv) Mwanaume yeyote mwenye kikuku (wristband) hata kama ni mheshimiwa, huwa ndoa yake inamsumbua,

v) Dera ni nguo mbaya zaidi. Sio nguo ya heshima, mpango wote wa kando huvaa dera.

vi) Mtindo wa kusherehekea wa Erling Haaland ni ishara ya waabudu shetani

vii) Ikiwa mke wako ana tattoo kwa shingo, kifua, miguu, mikono, mapaja, basi jiandae kushare na watu.

viii) Mwanamke ambaye ametoboa pua hana ndoa dhabiti.