Msanii maarufu wa nyimbo za injili anayetokea Kigoma Tanzania Christine Shusho, amechangia maoni yake kuhusu msanii mwenza nyota wa nyimbo za bongo Diamond Platinumz ya jinsilivyoingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza.
Kwenye mahojiano yake ya moja kwa moja na SPM BUZZ Shusho alieleza kuwa anaunga mkono sana swala la ubunifu.
Alieleza kuwa nchi ya Tanzania ni nchi ambayo inashiriki sana kwa ubunifu hasa katika sanaa ya muziki na kusema kuwa anaunga hilo mkono.
Shusho alisema kuwa, ikiwa kuingia jukwaani kwa msanii Diamond akiwa ndani ya jeneza ni mbinu ya ubunifu basi anaunga hilo mkono kwa;
"Naheshimu tasnia nzima ya sanaa Tanzania maana ni wabunifu sana,kwa hivyo chochot wafanyacho ikiwa ni ubunifu naunga mkono."
Haya yanajiri baada ya siku nne zilizopita ambapo msanii huyo Diamond Platinumz aliingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza katika hafla ya bendi ya wasafi.
Mnamo Septemba 11, Mwimbaji huyo wa nyimbo za Bongo, aliwasisimua mashabiki wake kwa onyesho la kutisha mjini Lindi,wilaya ya Raungwa ambako alipanda jukuani akiwa amebebwa kwenye jeneza .
Majeneza kadhaa yalibebwa hadi jukwaani na wanaume waliovalia mavazi ya kidini yenye kofia kama vile wanafanya aina fulani ya tambiko la kishetani.
Utendji huu uliwafanya wahafidhuni wengi kumhutumu Platinumz kuwa naabudu shetani.
Hata hivyo jambo hili lilipelekea msanii huyo kukiri kuwa alikuwa amehofia zaidi kuigiza akiwa ndani ya jeneza hilo
"Kutoka kwenye jeneza kulikua tukio la kichaa jana usiku,niliogopa sana!"
Tamasha hilo la wasafi festivals hushirikisha wasanii mblimbali waliosainiwa na Wasafi Records pamoja na wanamuziki wengine mashuhuri kutoka Tanzania na muziki wa afrika mashariki