Msanii Mbosso Khan kutokea Wasafi aliwakosha mashabiki usiku wa wikendi wakati wa tamasha la Wasafi mjini Songea.
Msanii huyo aliingia jukwaani kwa staili nyingine tofauti kabisa ambayo ilikuwa na ubunifu wa kiwango kingine.
Mbosso ambaye hivi majuzi ameachia wimbo wa Sele akimshirikisha Chley aliiangia na wimbo huo ambao unazungumzia vilevi.
Akipanda kwenye ngazi za jukwaani, Mbosso alikuwa amejifunga taulo jeupe huku mdomoni ameweka sigara kubwa na kutoa moshi huku kichwani amevalia kofia ya Waislam kabla ya kuwekewa wimbo huo wa Sele.
“Mirungi Mishisha, mibangi Seleman,” sehemu ya wimbo huo iliimba.
Mbosso ambaye aliwafurahisha mashabiki ambao walipiga kelele za kumkaribisha jukwaani kwa sekunde kadhaa alipakia kipande hicho kwenye Instagram yake ambapo mashabiki pia waliachia maoni wakisifia ubunifu wake.
“Uliua sana Mzee Selemani ,” Bosi wake Diamond Platnuzm alimhongera.
“Unyama ni mwingi sana🔥🙌🔥” mwigizaji Wema Sepetu alimwambia.
“SMASH BANGER 🙌🔥🙌🔥🙌🙌” Produsa S2Kizzy alisema.
Katika tamasha la Wasafi mwaka huu, wasanii wengi wameonekana wakija na ubunifu wao wakielekea jukwaani katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Wiki jana, tuliripoti kwamba msanii Diamond Platnumz aligonga vichwa vya habari baada ya kuingia jukwaani akiwa amebebwa ndai ya jeneza kama maiti.
Awali, msanii Whozu aliingia jukwaani akiwa amevalia mavazi kama mwehu vile huku usoni amejipodoa kwa vitu ambavyo vilimuonesha kama mtu aliyejeruhiwa.
Yote haya wasanii wameyafanya kwa ajili ya kunogesha shoo zao lakini hatua hizo zimepata mapokezi yenye maoni kinzani kutoka kwa mashabiki wao.