logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nadia Mukami avikwa taji la malkia wa muziki Afrika Mashariki, Zuchu aona vumbi Afrimma

“MSANII BORA WA KIKE AFRIKA MASHARIKI @afrimma 2023!! WE WOOOON🇰🇪. Asante @afrimma,” Mukami aliandika.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 September 2023 - 10:34

Muhtasari


  • • Mukami alikuwa anawania tuzo hiyo ya mwaka 2023 na wasanii wakali kama Zuchu na Maua Sama kutokea Tanzania.
  • • Akiandika kuhusu ushindi huo, Mukami aliwashukuru mashabiki wake waliomwaminia na kujitangaza rasmi kuwa ndiye malkia.
Nadia Mukami

Msanii wa kizazi kipya kutoka Kenya, Nadia Mukami ndiye rasmi malkia wa muziki wa kizazi kipya katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hii ni baada ya msanii huyo kushinda tuzo ya Afrimma ya msanii Bora wa kike usku wa kumkia leo katika hafla ya kutolewa kwa tuzo hizo.

Mukami alikuwa anawania tuzo hiyo ya mwaka 2023 na wasanii wakali kama Zuchu na Maua Sama kutokea Tanzania.

Akiandika kuhusu ushindi huo, Mukami aliwashukuru mashabiki wake waliomwaminia na kujitangaza rasmi kuwa ndiye malkia.

“MSANII BORA WA KIKE AFRIKA MASHARIKI @afrimma 2023!! WE WOOOON🇰🇪. Asante @afrimma,” Mukami aliandika.

Mashabiki wa mjasiriamali huyo wa Sevens Creative walimhongera wakisema kwamba ni mwaka ambao ametia for a Zaidi katika muziki wake, baada ya kuonekana kulegeza Kamba alipopata mtoto mwaka jana.

“Hongera Muembu wetuuuuu! Je, wanaona jinsi wanawake wa Embu walivyo na bidii?? Wanaweza!!? 😂😂🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾 Unastahili kabisa haya na ZAIDI Nadia. Endelea kukanyaga pedali hiyo ya gesi,” mtangazaji Mwalimu Rachel alimhongera.

“Hongera, Nadia, kwa kushinda Tuzo ya Afrimma 2023 ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki! Haya ni mafanikio ya ajabu na ushahidi wa talanta yako ya kipekee na bidii. Kujitolea kwako kwa ufundi wako kumezaa matunda, na unastahili kutambuliwa hivi. Muziki wako umegusa mioyo ya watu wengi, na mtindo wako wa kipekee na sauti yako yenye nguvu imevutia hadhira ulimwenguni pote. Tunajivunia sana na tunasubiri kuona ni mambo gani ya ajabu utakayotimiza katika siku zijazo. Endelea kuangaza na kuwatia moyo wengine kwa kipaji chako cha ajabu. Kwa mara nyingine tena, pongezi kwa tuzo hii inayostahili!” mwingine kwa jina Don Fiddie alisema.

Itakumbukwa Nadia pia ndiye msanii wa kizazi kipya wa Kenya pekee aliyeteuliwa kuwania tuzo za Trace ambazo zitafanyika hivi karibuni kwa mara ya kwanza barani Afrika, jijini Kigali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved