Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Kenya Nonini aliomba msamaha kwa Wakenya kwa kuunga mkono serikali ya sasa na baadhi ya viongozi wa kisiasa.
Katika ukurasa wake rasmi wa X, mwimbaji huyo wa genge alisema kuwa mambo hayaendi sawa mwaka mmoja tangu utawala wa sasa uchukue husukani.
"Tukiangalia nyuma jinsi nchi yetu inavyoenda mwaka chini ya mstari na serikali hii. Nataka kuwashirikisha WAKENYA kwa sauti kubwa kwa kuunga mkono serikali hii na baadhi ya viongozi unaowafahamu,” aliandika Nonini.
Aidha alisema yuko tayari kwa upinzani atakaopokea lakini akabainisha kuwa alikuwa na ujasiri wa kukiri kuwa viongozi hao wamefeli Wakenya.
“Inaitaji mtu mwenye nguvu kukiri walikosea na niko tayari kwa matusi yoyote hapo kwa maoni lakini angalau niko bold enough Kukubali mambo Kenya sio poa na baadhi ya viongozi wetu wametuangusha Sana. Poleni sana wakenya wenzangu,” mwanamuziki huyo aliongeza.
Hizi hapa baadhi ya hisia za Wakenya;
Mutwiri:Takes an even bigger man to own up to mistakes. They ran a very deceptive campaign, making all the right noises but it's taken just a year to reveal themselves as con artists/wash wash merchants they always were. 'Of importance is life'
David: It's very true. Things aren't good in this country. It's only a zombified person who can't see we are headed in the wrong direction.
fearless: Apologies accepted bro ...we all make mistake
Terry:The problem started when they elected uhuruto and Tano tena script was worse ,then came hustler nation worsest,now we are paying heavily weather we voted or no