Mkuza maudhui nchini Kenya Thee Pluto amepoteza akaunti yake ya TikTok kwa kile anachodai kuwa ni kosa la 'kipumbavu ambalo hakuwahi kulijua'.
Pluto anajilaumu kwa kupoteza akaunti yake ya TikTok ambayo ilikuwa na wafuasi zaidi ya 977K.
"Habari marafiki na familia leo nikashiriki nanyi habari mbaya lakini leo hali inanilazimisha kuwaambia najisikia vibaya siwezi kulia tuliambiwa wanaume msilie," Pluto alisema.
"Akaunti yangu ya TikTok yenye wafuasi 977k imefungwa, makosa sikujua kama hili ni kosa ." “Kuna kitu niliwapa marafiki 3 au 4 wakaniomba namba yangu nikamjibu wakaniambia WhatsApp, kisha nikaweka namba yangu 0994...hivo, sikujua hutakiwi kufanya hivyo hutakiwi kushiriki mawasiliano yao ni kuwa akaunti yangu imefutiliwa mbali ni vizuri kwamba nimejifunza" "Sasa imesimamishwa, imepigwa marufuku.
Ilikuwa ni akaunti ambayo nilifungua nyuma mwaka wa 2018 na nilikuwa karibu milioni" akishangaa kuhusu hasara yake.