logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rapa Sosuun asimulia kilichosababisha penzi lake na msanii Kenrazy kusambaratika

Sosuun alisema kwamba baada ya Amani kushindwa kupatikana, waliamua kuachana tu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 September 2023 - 12:00

Muhtasari


  • • “Kitu ambacho siwezi kukifanya ni kuzungumza vibaya kumhusu Kenrazy, ni baba kwa watoto wangu," Sosuun alisema.
Kenrazy na Sosuun

Rapa wa kike ambaye alikuwa anafnaya vizuri kwenye gemu miaka michache iliyopita, Sosuun kwa mara ya kwanza amesimulia kinagaubaga kilichosababisha penzi lake na mpenzi wake wa muda mrefu Kenrazy kusambaratika, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kupasua mbarika kwamba hawako pamoja tena.

Katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini, Sosuun alisema kwamba ni kweli yeye na Kenrazy si wapenzi tena licha ya kwamba walishajuana tangu wakiwa wadogo miaka mingi iliyopita.

Aliashiria kwamba mawimbi yalizidia jahazi la penzi lao na ikabidi tu kila mmoja aanze kujishughulisha na hamsini za kwake, lakini akashiria kwamba pengine Kenrazy ndio alikuwa hataki licha ya juhudi zake kujaribu kuleta Amani kwenye ugomvi wao.

“Ni maisha, chochote kilichotokea kilitokea. Unajua wakati mwingine unajatibu kurekebisha lakini haiwezi. Kila mtu sasa anaendelea na maisha yake na siwezi sema kwamba tuko pamoja. Hatuko pamoja,” Sosuun alisema.

“Ni jambo la kushangaza kwamba mtu ambaye anaonekana muongeaji huwa ndiye mbishi lakini ukweli ni kwamba mtu anayeongea sana ndiye anayejaribu sana kutafuta mwafaka,” aliongeza.

Sosuun alisema kwamba baada ya Amani kushindwa kupatikana, waliamua kuachana tu na akaapa kwamba kwamba kama kuna kitu ambacho hawezi kukifanya ni kuongea mabaya kumhusu Kenrazy.

“Kitu ambacho siwezi kukifanya ni kuzungumza vibaya kumhusu Kenrazy, ni baba kwa watoto wangu, ni mwanamume mzuri na pia ni mtu mwenye heshima sana, tunaheshimiana na ako vizuri katika masuala ya kunisaidia malezi,” Sosuun aliongeza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved