Leo ikiwa ni Alhamisi, siku ambayo watu wengi hujikumbusha matukio ya nyuma, mashabiki mitandaoni wameibua video wakati msanii Diamond alikiri wazi kwamba wimbo wake wa Mawazo aliouachia 2014 alimwandikia aliyekuwa mpenzi wake kipindi hicho Jaqueline Wolper.
Katika video hiyo, Diamond alikuwa ameketi kwenye mahojiano akijaribu kunyoosha maelezo kuhusu kilichomchochea kuandika wimbo huo.
Diamond alikiri wazi kwamba hata Wolper mwenyewe alijua kwamba ujumbe wa wimbo huo ulikuwa umeelekezwa kwake.
“Mawazo nilimuandikia Wolper. Huo wakati tulikuwa tuna’date. Mimi nikuambie kitu kimoja, mimi ni mtu Fulani ambaye nakuwa na mapenzi mengi sana. Halafu nikimpenda mwanamke najua kabisa nakuwa mjinga sana,” Diamond alisema.
Alisema kwamba kilichomfanya kuandikia Wolper wimbo huo wa kudai ana mawazo hata kutamani kulewa ili kuyapunguza ni baada ya muigizaji huyo wa zamani kumtenda.
“Ilitokea kwamba kuna vitu Fulani alikuwa amenifanyia hivi nikawa sivielewi. Kwa hiyo nikiwa namuandikia wimbo ule nilikuwa navuta hisia zangu nikisema ‘sikujua mapenzi ni balaa tena ni maradhi ya moyo ukipenda, utu wangu una thamani, ina maana kweli haukuvijua’ ndio nilikuwa namwambia ina maana hata ustaa wangu hakuuona. Wolper yeye mwenyewe analijua hilo,” Diamond alisema kwenye mahojiano hayo.
Itakumbukwa kwa kipindi hicho mwaka 2014, Diamond ndio alikuja kumsaini msanii wake wa kwanza kwenye lebo yake ya WCB Wasafi β Harmonize.
Baadae Wolper alikuja kuwa ndiye mwanamke wa kwanza maarufu kutoka kimapenzi na Harmonize japo uhusiano wao pia haukwenda sana.
Baada ya Harmonize kuachana na Wolper, kuliibuka na uvumi kwamba Diamond ndiye alisababisha kuachana kwao kwa kujaribu kurudiana tena na Wolper.
Hata hivyo, uvumi huo haukukolea na baadae Harmonize alinasa penzi la Muitaliano Sarah.
takumbukwa kwa kipindi hicho mwaka 2014, Diamond ndio alikuja kumsaini msanii wake wa kwanza kwenye lebo yake ya WCB Wasafi β Harmonize.