logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rayvanny ajawa huzuni baada ya jukwa la ndoto zake alilotumia mamilioni kujenga kuporomoka

Alifichua kuwa alitumia Tsh70M kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo na hata alitafuta huduma za wahandisi bora ili kufanikisha ndoto yake.

image
na Samuel Maina

Burudani01 October 2023 - 08:16

Muhtasari


  • •Rayvanny alitazamia kutumbuiza akiwa amepanda boti ndani ya bwawa lililojengwa uwanjani lakini ndoto hiyo yake ilikatizwa baada ya bwawa hilo kuporomoka.
  • •Alidokeza kulikuwa na mchezo mbaya kwenye tukio hilo kwani kuna mtu alitoboa shimo kwenye bwawa hilo na kufanya ukuta kuwa dhaifu.
CEO wa Next Level Music

Staa wa bongo Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny ni msanii mwenye huzuni baada ya jukwaa la bwawa la maji alilokuwa amejenga kuporomoka baada ya kujazwa maji.

Bosi huyo wa lebo ya Next Level Music alikuwa amepanga kuwatumbuiza mashabiki wake katika mkoa wake wa nyumbani, Mbeya akiwa amepanda boti ndani ya bwawa lililojengwa uwanjani lakini ndoto hiyo yake ilikatizwa baada ya bwawa hilo kuporomoka.

Katika taarifa ya kusikitisha Jumapili asubuhi, msanii huyo wa zamani wa WCB alifichua kuwa alitumia zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania (Ksh 4M)  kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo na hata alitafuta huduma za wahandisi bora ili kufanikisha ndoto yake.

“Hii show niliokua nimepanga na team Yangu ilikua ni show ya ndoto yangu nimeiota kwa muda mrefu sana yani ( Kuweka maji na kuingia na Boat) lakini sehemu ya uwanja wa show Ilikua ndoto yangu kufanya show ya tofauti nyumbani kwangu , Ambayo muda huu nilikubali kutumia kiasi. kikubwa sana cha pesa kivyovyote vile ili nifanikishe, Hua ninapofanya wazo kwa umakini mkubwa sana ndio hua tunautanguliza mbele yani licha ya kutafuta ma Engineer na watu waliobobea kwenye sekta ya matengenezo ila PLAN YANGU YOOTE HAIKUFANIKIWA ���������,” Rayvanny alisema kupitia Instagram.

Aliambatanisha maelezo yake na video inayoonyesha ujenzi wa bwawa hilo tangu mwanzo hadi karibu kukamilika kisha kuporomoka.

Kulingana na video hiyo, bwawa lilikuwa tayari limekamilika na boti ambayo Rayvanny angetumbuizandani yake  ilikuwa imeagizwa na ilikuwa ikisubiri kufanyiwa majaribio kwenye bwawa hilo wakati  tukio la bahati mbaya lilipotokea. Mwimbaji huyo alidokeza kulikuwa na mchezo mbaya kwenye tukio hilo kwani alishuku kuwa kuna mtu ambaye alitoboa shimo kwenye bwawa hilo na kufanya ukuta kuwa dhaifu.

“Team na mimi wote tuliingiwa na majonzi makubwa sana ikabidi nianze kuwafariji hadi hakija aliandika kitu wakati ukweli ni mambo ambayo yalitangaza kuwaambia wakuu, kwamba taarifa na kujiridhisha kua kazi imekamilika nikapata kazi ya kutafuta maana swala letu lilikamilika na tukawa tunasubiri ya boat. ila watu wasio kua na nia njema pia waliweza kulikamilisha jaribio hilo Maana Upande uliod ulitobolewa mashimo chini kipindi hiki tuko busy na matengenezo mengine ya Idea yetu!!! ," alisema.

Hata hivyo alidokeza kuwa tayari amejifunza kukubali changamoto zinapokuja kwani damia zitakuwa sehemu ya maisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved