Mcheshi wa Kenya Flaqo amejibu shutuma kutoka kwa Andrew Kibe kuhusu zawadi yake ya hivi majuzi ya siku ya kuzaliwa kwa mpenzi wake, Keranta.
Katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wake wa Instagram, Flaqo alifafanua kuwa ingawa video ya zawadi hiyo ilikuwa imepangwa mapema, Keranta hakujua kuhusu zawadi ya gari hilo huku akipuuza ukosoaji wa Kibe.
MMoja wa mashabiki wake alimuuliza kuwa;
"Kife alisema mlipanga surprise ati sisi ndio mlitusurprise fact or no?" shabiki aliuliza.
Huku akijibu swali la shabiki huyo Flaqo alionekana kumjibu Kibe kwa matamshi yake.
"Huo ulikuwa uchambuzi mbaya sana Omera buana... Ni dhahiri kwamba sote tulipanga surprise kwa maudhui yake ya youtube, alijua kamera zinaenda pia kwa video ya kushtukiza... ndio maana alikuwa na sauti na vipodozi kwa maudhui yake isipokuwa mlitaka ashuke kama ule. msee wa 'tunaanza usiku' M, what she didn't know is what the video is about… izi vitu ni obvious omera mmeanza kuniangusa bwana," Flaqo alijibu.
Flaqo alimshangaza Keranta mnamo Jumanne, Oktoba 3, alipomzawadia Nissan Note yenye thamani ya Ksh650,000 kwa ajili ya kutimiza miaka 22.
Video hiyo iliyoshirikiwa kwenye akaunti zao za Instagram ilionyesha wanandoa hao wakianza sherehe ya kuzaliwa kwa tarehe ya picnic kabla ya kuhamia lango lililofungwa.