Staa maarufu wa Afrobeat Davido alivuma mtandaoni saa chache baada ya kuitwa na mcheshi mkongwe wa Nigeria, AY Makun, ambaye alimdhihaki kwa kuwa na watoto wengi na wanawake tofauti wakati wa shoo wikendi iliyopita.
Kwa mujibu wa mchekeshaji huyo aliyeonekana kufanya utani kwa kutumia jina la Davido na sakata la kuandamwa na mimba nyingi kutoka kwa wanawake mbalimbali siku za hivi karibuni, alivuka mipaka na kudai kwamba alishangaa uwezo huo mkubwa wa Davido licha ya kile alikitaja kuwa msanii huyo ana uume mfupi.
Hatimaye mwimbaji huyo wa Nigeria amejibu maoni ya AY Makun kwa kuchapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, akibainisha kuwa maisha kamwe hayapendelei watu wema.
Hapa kuna sehemu ya maoni ya Davido kwenye mtandao wa X, awali ukifahamika kama Twitter:
"Maisha haya hayana neema kwa watu wema wakati mwingine … hata hivyo masomo yamepatikana,"
Hata hivyo, baada ya video za utani wa AY Makun akimponda Davido kusambaa mitandaoni, mcheshi huyo aliingia mtandaoni na kuomba msamaha.
Lakini majibu ya msanii huyo wa Afrobeat yamewafanya watu wazungumze baada ya kudondosha picha yake akipindua kidole chake cha kati na maoni yanayosomeka:
"Hapana, si Leo" kuonesha kwamba dhihaka hiyo bado inagali mbichi kwake na hayuko tayari kukubali msamaha wa aina yoyote kutoka kwa AY.
Kipande cha video cha AY Makun akinyanyua OBO kilisambaa mitandaoni baada ya kufanya utani nyeti kuhusu uwezo wa Davido kuwapa ujauzito wanawake licha ya kuwa na uume mdogo.
Kwenye picha hiyo ya Davido, mashabiki wengi walifurika kutoa maoni yao, baadhi wakihisi kwamba AY alimkosea heshima Davido kwa kuingilia mambo yake ya ndani ambayo hata yanafaa kujulikana au kuzungumziwa na mke wake tu.