logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond na Nyashinski kutumbuiza mashabiki Nairobi katika Octobafest

Diamond anararajiwa kutumbuiza  wafuasi wake huku sherehe hizi zikileta pamoja wasanii wa Afrika Mashariki

image
na Davis Ojiambo

Burudani12 October 2023 - 12:25

Muhtasari


  • •Tamasha hili ni sherehe kubwa ya utamaduni wa Afrika Mashariki, inayoleta watu pamoja ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za maeneo yote ya muziki wa Afrika.

Mwanamuziki na nyota wa Bongo Tanzania Diamond Platnumz anatazamiwa kuwatumbuiza mashabiki wake mwishoni mwa mwezi katika uwanja wa Ngong Racecourse katika Oktobafest mjini Nairobi.

Tamasha ambalo linatarajiwa kuleta pamoja na kushirikisha nyota wa Kenya Nyashinski na John Frog wa Sudan Kusini.

Ann-Joy Michira, mkurugenzi mkuu wa uvumbuzi wa chapa hiyo ya  "OktobaFest alisema ni sherehe ya utambulisho wa kipekee wa Afrika Mashariki, na safu ya wasanii wa mwaka huu ni dhihirisho la kweli la utofauti wa vipaji vya muziki katika ukanda huu.

Tunayo furaha kuleta pamoja vipaji vya ajabu kama hivi kutoka Sudan Kusini, Tanzania, Uganda, na Kenya na tunatazamia watazamaji kushughulikiwa kwa tajriba zisizosahaulika.

Tamasha hili ni sherehe kubwa ya utamaduni wa Afrika Mashariki, inayoleta watu pamoja ili kufurahia ladha, sauti na tamaduni za kipekee za maeneo yote ya muziki wa Afrika.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved