logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Drake amzawadi shabiki aliyehudhuria shoo yake gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon (video)

"Nataka kusikia mshindi akipiga kelele.”" alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani13 October 2023 - 08:33

Muhtasari


  • • Baada ya Drizzy kugeuza ngoma, aliingiza mkono wake ndani na kuchimba huku na kule huku umati ukishangilia, alitangaza mshindi kuwa mwenye tikiti nambari "17482."
Drake

Rapa maarufu kutoka nchini Kanada amewakosha mashabiki wake baada ya kumpa mmoja wa mashabiki wake gari la kifahari aina ya G Wagon wakati wa shoo yake mjini Toronto, Kanada.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 36 alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha lake la 'It's All a Blur Tour' katika uwanja wa Scotiabank Arena katika mji wake wa asili, Toronto siku ya Jumamosi, alitoa zawadi ya Mercedes-Benz G-Wagon kwa shabiki asiyetarajia.

Badala ya kuchagua binafsi shabiki kwenye hadhira ya kwenda nyumbani na zawadi ya kifahari, Drake aliyefika kwa shoo hiyo akiwa amejipanga aliamua kuchagua ngoma ya bahati nasibu ambayo ilikuwa na nambari za tikiti za kipekee za waliohudhuria.

"Kwa hivyo, hivi ndivyo nitafanya: nitachagua tikiti ya ushindi kutoka kwa ngoma hii hapa," Drake alisema, wakati washiriki wa timu yake wakileta ngoma ya bahati nasibu kwenye jukwaa. "Nataka kila mtu awe kimya sana. Nataka kusikia mshindi akipiga kelele.”

Baada ya Drizzy kugeuza ngoma, aliingiza mkono wake ndani na kuchimba huku na kule huku umati ukishangilia, alitangaza mshindi kuwa mwenye tikiti nambari "17482."

Hatimaye, alimwona shabiki aliyekuwa akipeleka gari jipya nyumbani katika moja ya ngazi za juu za Scotiabank Arena.

Ipasavyo, alisema, "Wamezipata? Wao juu? Bora ulete punda wako hapa. Tutamtuma mtu huko aangalie tikiti hiyo."

Hata hivyo haijulikani ni modeli gani ya Mercedes-Benz G-Wagon ambayo msanii wa "Rich Flex" alitoa lakini kulingana na tovuti ya Mercedes-Benz, modeli ya kawaida inauzwa kwa $139,900 sawa na shilingi za Kenya 20,831,110.

Tazama video hii jinsi msanii huyo alifanya kufuru hiyo ambayo haijawahi tokea kwenye tamasha loote duniani;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved