Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kituo cha Furaha Fm nchini Tanzania amesimulia kilicho mfanya kumpa muingizaji Wema Sepetu Nafasi ya kuwa mtangazaji katika Kituo hicho.
Baada ya mahojiano ya moja kwa moja na wablogu Furaha Dominic mkuu wa radio hii alisimulia changamoto wanazopitia vijana wengi ndiposa alimchangua Wema Sepetu kuwa mmoja wa watangazaji watakao kuwa mfano mwema kwa kuwapa vijana mawaidha.
"Wema sepetu naelewa vyema kuwa yeye si mtangazaji mbali ni muingizaji mashuhuri wa vipindi ,ila kwenye kituo cha Furaha tuliona ni vyema awe mmoja wetu kwa vile tunaamini masahibu anayopitia yanawakuba vijana wengi na huenda akipata nafasi ya kuongea na vijana wengi huenda wakabadilika hio ndio furaha yetu",alisema .
Mkurugezi huyu kwenye mahojiana hayo pia alikiri kwamba baada ya kumkabidhi muigizaji Wema nafasi hiyo aliweza kufurahishwa na jambo hilo na kukubali kufanya kazi kwenye kituo hicho ili kuwapa wengi ushauri kupita changamoto nyingi alizokumbana nazo katika maisha yake kama muigizaji wa vipindi vya Bongo.
"Nilichangua Furaha FM kwa maana ndio Radio bora zaidi inayoelimisha jamii ,natumai pia watu wengi wananifahamu kama kioo cha jamii kwa hivyo ndio maana nikachangua stationi ambayo inapedwa na vijana hili tuweze kushauriana ",alisema Wema Sepetu.