logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tiwa Savage aahirisha shoo zake zote, afichua kupambana na virusi wiki za hivi karibuni

Hata hivyo, aiahidi kwamba tarehe mpya za matamasha yake zitatangazwa upya pindi atakapopata nafuu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 October 2023 - 08:33

Muhtasari


  • • "Kwa bahati mbaya, nitalazimika kuahirisha shoo zangu zote ikiwemo shoo yangu ya kwanza ambayo ingefanyika London,” alisema.
Tiwa Savage

Mkali wa Afrobeat wa Nigeria, Tiwa Savage, amesitisha kufanya muziki kwa muda kutokana na ugonjwa wa ajabu.

Malkia huyo anayetamba kwa wimbo wa ‘Koroba’alitoa ujumbe huo wa kuwakatisha tamaa mashabiki wake katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba amekuwa akipambana na virusi, jambo ambalo lilimlazimu kustarehe kwa muda mrefu wa kupumzisha sauti, kwa miezi kadhaa.

Savage alisema kwamba kwa bahati mbaya, pia atalazimika kuahirisha shoo yake ya kwanza kabisa ambayo ingefanyika mjini London, Uingereza.

“Kwa wanajeshi wangu wa Savage, nimekuwa nikipambana na virusi kwa wiki za hivi karibuni na hivi leo niliamrishwa vikali kuchukua mapumziko ya sauti yangu kwa miezi kadhaa ijayo. Kwa bahati mbaya, nitalazimika kuahirisha shoo zangu zote ikiwemo shoo yangu ya kwanza ambayo ingefanyika London,” alisema kwenye taarifa.

Tiwa Savage amekuwa akijulikana kila mara kwa maadili yake ya kazi, akitoa maonyesho ya nguvu kwenye maonyesho yake. Hata hivyo, umuhimu wa kutanguliza afya hauwezi kusisitizwa. Wasanii, kama wataalamu wengine wowote, wanahitaji kupumzika na kupona vya kutosha, haswa wanapokabiliana na maswala ya kiafya.

Hata hivyo, Tiwa alitangaza kwamba analazimika kuahirisha utendaji wake wote wa muziki kutokana na virusi hivyo.

Savage alisema kwamba kama ambavyo tangazo hilo limewasawijisha mashabiki wake, naye vile vile limemvunja moyo kwani hakutarajia kwamba tatizo hilo lingekuwa kubwa hivyo.

Hata hivyo, aiahidi kwamba tarehe mpya za matamasha yake zitatangazwa upya pindi atakapopata nafasi ya kuendelea na kutumbuiza kutoka kwa daktari wake.

“Nimevunjika moyo sana na hili lakini pia ninahitaji kuzingatia masharti ya daktari ili kuokoa kile kidogo kilichosalia katika sauti yangu. Naomba radhi, nawapenda nyote na naahidi kurudi kwa nguvu mpya kutumbuiza pindi nitakapopata nafuu kikamilifu,” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved