logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ninaposema nipigie unapohitaji chochote simaanishi pesa - Ezekiel Mutua afafanua

“Hapana daktari, pesa ni neno la kutia moyo,” Omondi MC’Onyango alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 October 2023 - 05:58

Muhtasari


  • • “Ninaposema "nipigie unapohitaji chochote," simaanishi pesa. Namaanisha maneno ya kutia moyo,” Mutua alisema.
Ezekiel Mutua

Mkurugenzi mkuu wa bodi inayosimamia hakimiliki za kazi za Sanaa nchini MCSK, Dkt Ezekiel Mutua amefafanua anachokimaanisha kila mara anapotoa ushauri kwa wale wanaohitaji misaada kumtafuta kwa njia ya simu.

Mutua kupitia ukurasa wake wa Facebook asubuhi ya Jumanne, alichapisha ujumbe wa utani akisema kwamba kwa njia moja au nyingine kumekuwa na mkanganyiko wa lugha gongana baina yake na watu ambao anawaambia kuwa wakihitaji usaidizi wasisite kumtafuta kupitia kwa simu.

Mutua aliweka wazi kwamba anapowaambia wanaohitaji msaada kumpigia simu, hamaanishi kwamba moja kwa moja ni kumaliza matatizo yao ya kifedha bali pia msaada au usaidizi unaweza kuwa kwa njia nyingine kama maneno ya kutia moyo na ushauri pia.

“Ninaposema "nipigie unapohitaji chochote," simaanishi pesa. Namaanisha maneno ya kutia moyo,” Mutua alisema huku akipakia picha yake akiwa na furaha na kicheko ghaya.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake kwenye mtanao huo walisema kwamba akishasema chochote, hilo lina maana kwamba hata tatizo la mkwamo wa kifedha limo kwenye  mabano ya ‘chochote’

“🤣🤣🤣... lakini chochote daktari....... Usituwekee kikomo wakati wa kukuita bwana,” Geoffrey Ogolla alimwambia.

“Hapana daktari, pesa ni neno la kutia moyo,” Omondi MC’Onyango alisema.

“Daktari nadhani wote wawili wanaweza kufanya vizuri zaidi; pesa pamoja na maneno ya kutia moyo basi tunayaita mazungumzo yenye matunda mengi na Daktari 😃” Joash Sych alimwambia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved