Ukurasa wa Naseeb Juniro, mwanawe Diamond na Tanasha unaoendeshwa na mamake Jumatatu umepakia picha ya mtoto huyo akionekana kuserebuka kwa madaha.
Ni picha ambayo imevutia maoni tofauti kutoka kwa watu wengi huku baadhi wakisema kwamba kando na mfanano wa shilingi kwa ya pili wa sura na babake, mtoto huyo pia kwa asilimia kubwa – kama sio mia – anaonekana kuiga nyendo na tabia za babake.
Naseeb Junior ambaye ni kipenzi cha Mama Dangote alitokea akiwa amevishwa kisanii kichwani amefunga bandana yenye rangi sawia na ya suruali yake.
Kwa juu pia alipiga pamba nyeupe ambayo iliwiana kwa rangi na viatu na kumalizia shingoni kwa mikufu ghali iliyojimwaya na kutiririka kwenyewe kwenye kifua.
Alimalizia machoni na miwani ya kisanii vile vile.
Mtoto huyo alionekana kutembea mbele kwa madaha wakati wa kuchukuliwa picha hiyo, na kuzua taswira kama ya babake – Diamond Platnumz, msanii wa maswagg.
“Mnyamwezi wangu huyoooooo,” Esma Platnumz aliandika.
“Jamaa yake haongei sana.... ila mtazame...... anatabia ya nyota kweli..... 🔥🔥🔥🔥🔥... lamination halisi ya Simba [Diamond] mwingine aliandika.
“Nilidhani ni diamond mwanzoni.... Lol photo copy nayo 😍😍” Faith Ndinda alisema.
“Yaan huyu mtoto anafanana na baba yake mpka kucha duh!” Josephine Augustino alikomenti.