Mwanadada mkenya, Alicia, amemtaka mumewe kufuata nyayo za mwanamuziki Bahati baada ya kumtunuku mkewe kwa kutimiza miaka saba ya ndoa.
Katika video inayovuma, mwanamume huyo alikuwa ameketi kwenye kochi huku mkewe akimrekodi na kumwambia jinsi Bahati alivyotekeleza shughuli hiyo ya kumzawadi mkewe.
Alimwomba mumewe amwige mwanamuziki Kevin Bahati baada ya kumpa mke wake zawadi za kifahari kwa ajili ya maadhimisho yao ya mwaka.
"Unajua Diana amenunuliwa gari la Range Rover na bwana yake Bahati?Unafaa kuchukua mfano wa Bahati,"
Bahati na mkewe walikuwa wakisherehekea miaka saba wakati mwanamuziki huyo alipotoa zawadi za kifahari.
Mwanamuziki huyo alitajwa kuwa mume bora na mashabiki kwa kumwonyesha mke wake mapenzi kwenye mitandao ya kijamii.
TikToker Alicia alimwomba mume wake aanze kumtunuku kama mpenzi wake.Alifahamu fika kuwa mume wake hakuwa na uwezo wa kununua gari la aina hiyo ndiposa akamwambia angalau amnunulie zawadi ya baiskeli.
"Hata kama hautanipatia Range Rover anza na baisikeli,unajua hiyo gari ni Shilingi milioni 19,"alisisitiza.
Hata hivyo mume huyo alionekana kukwepa ombi la mumewe kwa kudai kuwa zawadi hizo ambazo watu wanaonyesha mitandaoni huenda sio za kweli.
Watumiaji wa mitandao,hata hivyo walitoa maoni yao,huku wakimkosoa vikali mke huyo wakimwambia kuwa ni vyema kuridhika na maisha ya mumewe bila kutamani ya watu.
Hivi majuzi, mwanamuziki Bahati, amevuma kwenye mitandao ya jamii, akionekana kumzawadi mkewe Diana zawadi mbali mbali wakati wakiadhimisha miaka saba ya ndoa.
Zawadi ya Diana ya gari hilo ilifuata sherehe za kitamaduni ambazo mwanamuziki huyo alienda kumlipia mkewe mahari,wakati ambapo wanajiandaa kufunga pingu za maisha.