Mpenzi wa Rayvanny, Fahyvanny ametoa maoni yake kwamba wanawakec weupe wana bahati sana katika mapenzi kulinganishwa na wanawake weusi.
Akizungumza kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari, Fahyma alisema kwamba hata yeye hajawahi elewa ni kwa nini sura za wanawake weupe zina asilimia kubwa ya kuwavutia wanaume kuliko sura zenye rangi nyeusi.
Fahyvanny alisema kwamba anamjua vyema mrembo aliyechukua nafasi yake kwa muda [Paula] kwamba ni mweupe na pengine weupe wake ndio ulimchanganya kidogo baba wa mtoto wake lakini baada ya kufunguka macho, aligundua kwamba weupe na mapenzi haviendani kwa sana.
“Unapendwa lakini sasa tukubali au tukatae ni kwamba wasichana weupe wanapendwa Zaidi. Sina maana mbaya lakini hata mwanamume yeyote yule aliye na mwanamke mweusi ndani yake aliyekuwepo ni mweupe,” Fahyvanny alisema.
Mama huyo wa mtoto mmoja tangu warudiane na Rayvanny mapema mwaka huu, wamekuwa wakipaishana kwa mapenzi mubashara huku Rayvanny kwa wakati mmoja akinukuliwa kukiri kwamba endapo atashawishika kumuacha mpenzi wake safari hii basi watu wampige mawe hadi kufa.
Rayvanny amekuwa akionesha mapenzi yake kwa mama wa mwanawe huku akimtumia pia kwenye baadhi ya video za ngoma zake kama vixen wa video jambo ambalo limewafurahisha mashabiki wao.
Kwa sasa, Fahyvanny amebadilisha jina la utambulisho wake kwenye Instagram na kujiita Mr Chui, kwa maana kwamba ni mke halali wa Rayvanny anayejiita jina la Chui.