Kwa mara ya kwanza msanii Nandy kutoka +255 amefunguka kwa nini mwaka huu hakuufanyika tamasha lake la kila mwaka – Nandy Festival.
Katika mazungumzo na wanahabari, Nandy alisema kwamba alichukua mapumziko kwa ajili ya kuwa na mwanawe lakini akafichua kwamba maandalizi ya Nandy Festival mwaka kesho yameanza mapema na kuwa tamasha hilo litang’oa nanga mapema mwakani.
Nandy pia aliweza kuzungumzia ukaribu wake na msanii kutoka Kenya, Tanasha ambaye huenda akawa mmoja wa wasanii watakaoburudisha mashabiki kaitka tamasha hilo.
Nandy aliwashangaza wengi kwa kufichua kwamba yeye na Tanasha wamekuwa mashosti kitambo kabla hata mrembo huyo hajaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond.
“Ukaribu wangu mimi na Tanasha, mimi na yeye tumeongea kabla hata hajawa na mahusiano na Diamond, kwa sababu mimi ni zamani kipindi cha Hallelujah naimba na Willy Paul naenda Kenya. Tanasha nilikuwa naongea na yeye. Mimi na yeye ni marafiki Mungu kamjaalia kawa mama na mimi nimekuwa mama na tukikutana huwa hatuongelelei mambo ya familia sana bali huwa tunaongelelea kuhusu taaluma ya muziki,” alisema.
Msanii huyo alikuwa anaelezea kinagaubaga kuhusu kuonekana kwake kwenye siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Naseeb Junior ambayo ilifanyika jijini Tanga ambapo pia Diamond alikuwepo na alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa vile vile.
Diamond na Tanasha walianza kuchumbiana mapema mwaka 2019 kabla ya kuachana mwaka mmoja baadae.