Seneta maalum wa chama tawala cha UDA Karen Nyamu,ametuma ujumbe wa heri kwa watahiniwa ambao wanafanya mitihani yao ya KCPE na KPSEA mwaka huu.
Nyamu, alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumatano Octoba 1,akiwatakia watahiniwa wote kila la heri kwa mitihani yao.
"Kwa watoto wetu wote wapendwa wanaofanya mitihani yao jijini Nairobi na kwingineko, ninawatakia kila la kheri," alinakili.
Seneta huyo,vile vile aliwatia moyo watahiniwa kwa kusisitiza kuwa mitihani ni njia mojawapo ya kutimiza malengo na ndoto zao maishani.
"Mitihani itakuleta karibu zaidi na lengo lako na mafanikio. Heri njema!"alisisitiza.
Heri za Nyamu zilipokelewa kwa moyo mkunjufu na baadhi ya mashabiki ambao humfuatilia katika mitandao ya jamii,na ambao pia ni wazazi wa watahiniwa,wakimshukuru kwa kuwakumbuka watahiniwa wote nchini.
Hata hivyo, Baadhi ya mashabiki hao, walionekana kumpiga vijembe Senata Nyamu kwa kutuma jumbe za heri kwa watahiniwa siku ya kukamilisha zoezi hilo.
Liz Wambui, alimuuliza Nyamu:
"Kuwa serious, unawakumbuka leo wakati wanamaliza,🤣🤣ulikuwa wapi Jumatatu?" aliuliza.
Mitihani ya KCPE pamoja na ile ya KPSEA ilingoa nanga Jumatatu Oktoba 30, ambapo inatarajiwa kukamilika Jumatano Novemba 1.
Wizara ya elimu ikishirikiana pamoja na polisi walihakikishia wakenya,kuwa usalama utaimarishwa kila sehemu ya mitihani ili kuleta utulivu wa zoezi hilo.
Maafisa wa polisi zaidi ya elfu 60,00 walitumwa katika vituo vya mitihani kuhakikisha visa vya udanganyifu,havishuhudiwi.
Japo visa mbali mbali vilishuhudiwa,vikiwemo watahiniwa kukosa mitihani,wizara ya elimu kwa mara ya kwanza ilihakikisha kuwa watahiniwa hao watapata nafasi ya kufanya mitihani hiyo baadaye.