Naya, mtoto wa familia ya kistaa, Billnass na Nandy akiwa na umri wa mwaka mmoja tu, tayari ameshakuwa milionea mpya mjini.
Hii ni baada ya mtoto huyo kupokea ubalozi wake kwa kampuni moja na wazazi wake kwa furaha wamepeleka mitandaoni kumsherehekea kwa kuingiza hela zake za kwanza baada ya mwezi mmoja.
Miezi miwili iliyopita, wakati anamtambulisha rasmi mitandaoni, Nandy alionesha wafuasi wake sura ya mtoto huyo mzuri, ikiwa ni siku yake ya kufikisha mwaka mmoja na kwa kiasi kikubwa alikuwa na mchanganyiko wa sura za wazazi wake wote, Billnass aionekana kukolea Zaidi.
Awali kupitia ukurasa wa Instagram wa mtoto huyo – Naya Bill – Nandy ambaye ndiye anaendesha akaunti hiyo alipakia video ya mwanawe akiwa ameshikilia moja ya bidhaa inayokisiwa kuwa ndiyo amejukumiwa kuitangaza kama balozi wa mauzo.
Mbele yake kuliuwa na burunguti kubwa na nono la noti na mamake alithibitisha hilo akisema kwamba ndio mwezi wa kwanza na tayari kuilichokuwa kikionekana mbele yake ndio mshahara wake wala hawajaribu kufeki maisha.
“Wikendi yenye furaha kwa Naya na rafiki yake. Hatimaye Naya anaanza rasmi kutambulisha taratibu balozi zake moja moja, na jana kapokea mshahara wake wa mwezi. Kanituma niseme stay tuned, ana jambo lake wikendi hii,” Nandy aliandika kupitia ukurasa wa Instagram wa mwanawe.
Billnass ambaye ni baba mtoto pia alikwenda kwenye akaunti hiyo na kutania akisema;
“Hivi si inatakiwa baba amshikie? [hela] zinahitaji uangalizi na ulinzi wa babake jamani.”
Kama hiyo haitoshi, mapema Ijumaa kupitia insta story yake, Nandy alipakia video hiyo hiyo akionesha furaha kiasi gani ameweza kulea na ndani ya mwaka mmoja na miezi michache tu tayari mwanawe ameanza kujisimamia mahitaji yake.
“Kale kafeeling mtoto wako kuanza kuingiza mpunga, Naya Bill hongera mwanangu,” Nandy alijivunia mwanawe.
Hata hivyo hatua ya kumtambulisha kwenye mitandao ya kijamii inakinzana na ahadi yake mwaka jana alipokuwa anaelekea kujifungua.
Nandy alisema kwamba asingetaka hata kidogo kumtambulisha mwanawe mitandaoni hadi pale atakapokuwa mtu mzima miaka 18 na kujichagulia maisha yake kama ya mitandaoni ama ya faraghani.