logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rotimi atumia Kiswahili kumtania Wolper baada ya kufanya challenge ya ngoma yake

“Kwa hali ya hewa hii watoto wangu vipenz vyangu ndo maBestie zangu wa kunifariji” aliandika.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 November 2023 - 10:14

Muhtasari


  • • Rotimi alicheka na kukiri kwamba kwa miaka michache ambayo amekuwa na Vanessa Mdee nchini Marekani, amejifunza machache kuhusu Kiswahili.
  • • “lol I learned a couple things over the years, sis😂! Najifunza, Asante Sana,” Rotimi alijibu.
Rotimi.

Shemeji wa Watanzania kutoka Marekani, Rotimi amewashushua watanzania baada ya kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha wakati anampongeza mmoja wa mashemeji zake, mwigizaji Jackline Wolper.

Picha lilianza pale Wolper alipakia klipu fupi kwenye Instagram yake akiwa na wanawe wawili na kwa umbali alikuwa anasikiliza na kucheza wimbo wa Rotimi.

Wolper, ama ukipenda mama P alisema kwamba kwa hali ya anga ambayo ni kijibaridi katika sehemu nyingi, alilazimika kukaa tu ndani na wanawe kujivinjari.

Kwa hali ya hewa hii watoto wangu vipenz vyangu ndo maBestie zangu wa kunifariji” aliandika.

Hapo ndipo watu wengi walifika na kuachia komenti zao na mmoja kati ya hao ni Rotimi mwenyewe ambaye alionesha furaha kwa shemeji yake kuonesha kuukubali wimbo wake.

Alimwandikia;

“Umetishaaaa dada.”

Akimjibu, Wolper alimpongeza Rotimi kwa wimbo huo mkali, tena kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

“Sawa shem Nyimbo kali kinoma haya mpe Dada hapo akupe habari ya haya Maneo yani nyimbo yako Niyakufunga Mwaka🙌besteeeee.”

Rotimi alicheka na kukiri kwamba kwa miaka michache ambayo amekuwa na Vanessa Mdee nchini Marekani, amejifunza machache kuhusu Kiswahili.

“lol I learned a couple things over the years, sis😂! Najifunza, Asante Sana,” Rotimi alijibu.

Komenti hii ilivutia maoni kadha wa kadha, baadhi wakicheka kwa furaha kwa shemeji yao kung’amua Kiswahili lakini pia wapo wengine waliosema kwamba huyo atakuwa ni mkewe Vanessa Mdee aliyeingia kwenye akaunti yake na kuandika kwa chapisho la Wolper.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya Watanzania;

“Muandiko wa vanessa huu😂😂” Tzdee alisema.

“aaaah weeeeee huyu n mpare kaandika😂😂😂😂😂😂😂😂” Mushy Spora.

“Hee huu sio mwandiko wako,” mwingine alimwambia Rotimi.

Ikumbukwe Rotimi ni msanii na mwigizaji kutoka Marekani mwenye asili yake nchini Nigeria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved