logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Erick Omondi aanzisha mchango wa kutoa mochwari mwili uliokwama kwa miaka 5

Tunahitaji zaidi ya laki saba ili kumzika marehemu Erick Omondi asema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 November 2023 - 09:33

Muhtasari


  • •Mchekeshaji Eric amesema kuwa iwapo watafanikiwa kumzika marehemu ataanzisha tena mchakato wa kuchanga hela ili kulipia karo watoto  wawili walioachwa na marehemu
Eric Omondi

Mchekeshaji  Eric Omondi ameazisha mchakato wa kuchangisha pesa hili kupumzisha mwili wa mwanaume  mmoja ambaye alifariki mwaka wa 2019 huku mwili wake ukiripotiwa kukaa mochwari kwa miaka tano.

Kulingana na ujumbe kwenye mtandao wake wa instagram Marehemu Eric Gori alifariki mwaka wa 2019 na mwili wake  hadi leo bado umo kwenye chumba cha kuifadhi maiti katika makafani ya Chiromo.

Eric amesimulia zaidi kwamba marehemu aliacha watoto wawili akisema kuwa familia yake imevumilia kwa miaka tano kwa kukosa hela za kumzika mpedwa wao.

"Nimewasiliana na wahudumu wa makavani ya Chiromo na kuwajulisha ili kutayarisha mwili wa marehemu ili tuweze kumpumuzisha jumatano iwapa tutafanikiwa kuchangisha zaidi ya laki saba zinazohitajika hili kuruhusiwa kuchukua mwili,"alisema Eric Omondi.

Mchekeshaji Eric amesema kuwa iwapo watafanikiwa kumzika marehemu ataanzisha tena mchakato wa kuchanga hela ili kulipia karo watoto  wawili walioachwa na marehemu.

Mchango huyo unatokea siku chache baada ya mwanablogu huyu kuonekana hivi majuzi akimsaidia mama aliyepoteza mtoto wake kumzika katika makaburi ya Langata.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved