Yvette aghadhabika baada ya kuambiwa gari lake mpya ni bonasi aliyopewa Bahati aliponunua Range Rover

Mama Mueni amenunuaNissan Note ya bluu wiki chache tu baada ya Bahati kumzawadia Diana Marua Range Rover ya bluu.

Muhtasari

•Yvette alionyesha picha yake akiwa amesimama mbele ya Nissan Note ya bluu na kudokeza kuwa hilo ni gari lake jipya.

•Katika jibu lake, mama huyo wa binti mmoja alionyesha wazi kwamba hakupendezwa na maoni hayo.

Yvette, Bahati, Diana Marua
Image: INSTAGRAM

Mfanyibiashara maarufu Yvette Obura alikuwa na habari za kusisimua za kushiriki na mashabiki wake mnamo siku ya Jumatano, Novemba 8.

Mama huyo wa binti mmoja alionyesha picha yake akiwa amesimama mbele ya Nissan Note ya bluu na kudokeza kuwa hilo ni gari lake jipya.

"Pesa kidogo nishanunua kadudu," Bi Yvette aliandika kwenye chapisho hilo na kuishukuru kampuni iliyomuuzia gari hilo.

Katika picha nyingine, mzazi mwenza huyo wa mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati alionekana akiwa ameshika funguo zinazoaminika kuwa za gari lililoegeshwa mbele yake.

Makumi ya wanamitandao wakiwemo mastaa wenzake walikusanyika kwenye chapisho lake kumpongeza huku wengine wakikejeli hatua hiyo. Mtumiaji mmoja wa Instagram alidai kuwa gari hilo lilikuwa bonasi ambayo Bahati alipewa baada ya kumnunulia mke wake wa sasa, Diana Marua gari aina ya Range Rover.

“Hiyo ndiyo zawadi Bahati aliongezewa baada ya kunua range,” @rosemary irungu alitoa maoni kwenye posti ya Yvette.

Katika jibu lake, mama huyo wa binti mmoja alionyesha wazi kwamba hakupendezwa na maoni hayo.

“mama mzima kama wewe huna akili!” Alijibu.

Tazama maoni ya watumiaji wengine wa mtandao;

@mrseedofficial: You played which song hapo ya kwanza.. am proud of you, congrats.

@officialkinuthia: Karibu to the Note team.

@eunnycharles: Hii ni marketing, mum Mueni has a big car

@isirengo: Congrats! Change colour kabla team Diana waanze ooh sijui umecopy gift number 7 bla bla bla…

@nipha.001: Ladies who get their own, I celebrate your win, congratulations.

Wanamitandao wamejaribu kulinganisha hatua ya Yvette kununua gari la bluu na hatua ya hivi majuzi ya Bahati ambapo alimzawadia mkewe gari aina ya Range Rover ya bluu.

Mwezi uliopita, mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alimshangaza Diana Marua na gari mpya kabisa ya Ranger Rover Vogue Autobiography, inayokadiriwa kugharimu takriban Ksh 19 milioni.

Baada ya kuliona gari hilo la kifahari la rangi ya buluu, Bi Diana Marua alilia kwa machozi ya furaha akikiri kwamba alikuwa haamini kwamba lilikuwa lake rasmi.

"Hii ni Ranger Rover Vogue Autobiography mpya. Hili ndilo toleo bora zaidi na hizi ni funguo za gari lako. Limefanyiwa ukarabati maalum kwa ajili yako, ndani ni rangi ya divai nyekundu iliyogeuzwa kukufaa na kila kitu ni cha kipekee na gari hili ni moja tu nchini Kenya, lako pekee,” Bahati alimwambia mkewe akimkabishi gari hilo.

Diana alijibu, “Nilifanya nini ili kustahili haya yote…Siwezi hata kuamini ... asante, Mungu,".

Hii ilikuwa zawadi namba saba ambayo Bahati alimpa mkewe wakwati wakisherehekea miaka saba ya ndoa yao.