logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mr Beast alikuja kuunda maudhui si kusaidia -KRG asema

Youtuba Mr Beast amecheza na fikra za wakenya na ili kuinua chaneli yake KRG afunguka

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 November 2023 - 06:51

Muhtasari


  • •Msanii huyo aliwataka wafuasi kwenye mitandao kukoma kumtaja ajitokeze kusaidia wakenya kama alivyofanya Youtuba Mr Beast

Msanii wa Kenya almaarufu KRG The Don  amepinga vikali mchango wa Youtuba Mr Beast aliyedaiwa kuchimba visima 52  akisema kuwa Youtuba huyo alikuwa akicheza  na akili za Wakenya hili kupata Wafuasi wengi Kwenye mtandao.

"Mr Beast alikuja Kenya kuunda maudhui ya chaneli yake wale si kusaidia kwa sasa amecheza na akili za Wakenya mpaka akafikisha wafuasi millioni 70 kwa mtandao wake kwa kucheza na fikra za watu,"alisema KRG.

Msanii huyo alisema hayo baada ya kuchapisha video moja Kwenye mtandao wake huku akimtaka Mr Beast kuacha kuchezea fikra za wakenya ili kupata wafuasi.

"Kusaidia hutoka kwa roho ya kila mwanadamu,si kwa kuchezea fikra za watu ili kujifanya uko na roho ya kusaidia, kujitafutia jina ili kujinufaisha kwa kupata wafuasi wengi,"alisema.

Msanii huyo aliwataka wafuasi kwenye mitandao pia  kukoma kumtaja ajitokeze kusaidia wakenya kama alivyofanya Youtuba huyo wa Marekani Mr Beast.

Kila mkenya afanye maendeleo yake kivyake maisha ni ngumu kwa kila mkenya mambo ya kunitaka kujitokeza kusaidia mkome kusaidia ni uamuzi wa mtu si kulazimishwa,"alisema.

Msanii huyo, anayejulikana kwa kuwa muazi na mtindo wake wa maisha, alisema kuwa utajiri wake si kwa ajili ya kufanya nia njema kama bilionea huyo wa Marekani. Aidha alifichua kuwa hana huruma kwa watu ambao hawako tayari kujiondoa kutoka kwa umaskini.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved