logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Koti la Michael Jackson lauzwa shilingi milioni 46.4 kwenye mnada

Koti hilo lilikuwa kati ya zaidi ya bidhaa 200 za kumbukumbu za muziki zilizouzwa London siku ya Ijumaa,

image
na Samuel Maina

Burudani11 November 2023 - 11:34

Muhtasari


  • •Koti hilo lilikuwa kati ya zaidi ya bidhaa 200 za kumbukumbu za muziki zilizouzwa London siku ya Ijumaa.

Koti la ngozi liliyovaliwa na Michael Jackson katika miaka ya 1980 limenunuliwa kwa £250,000 ($306,000). (Ksh 46,371,610)

Vazi hilo la rangi nyeusi na nyeupe, lililokuwa likivaliwa na mwimbaji huyo marehemu katika tangazo la Pepsi, lilitarajiwa kuuzwa kati ya pauni 200,000 na 400,000 katika mnada huo.

Koti hilo lilikuwa kati ya zaidi ya bidhaa 200 za kumbukumbu za muziki zilizouzwa London siku ya Ijumaa, ikiwa ni pamoja na koti la George Michael na kipande cha nywele cha Amy Winehouse.

Bidhaa zenye kuhusishwa na David Bowie, Oasis na The Beatles pia ziliuzwa mnadani.

Jackson alivaa koti hilo mnamo 1984, katika mfululizo wa kwanza wa matangazo ya biashara ambayo nyota huyo aliifanyia kampuni ya soda.

Matangazo hayo yanakumbukwa zaidi kwa tukio ambalo nywele za Jackson zilishika moto wakati wa kipindi cha upigaji picha, na kumwacha na majeraha mabaya.

Alikuwa amevaa koti tofauti wakati huo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved