logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa anusurika kukatwa uume wake baada ya mashine ya grinder kumuingia nguoni (video)

"Nilipotazama chini niliweza kuiona mahali pa mwisho ambapo ningeitaka," alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 November 2023 - 13:59

Muhtasari


  • • Katika klipu ya TikTok, mtunzi huyo aliyeonekana na sura ya kuogopa aligeukia kamera muda mfupi baada ya kutokea.
Mashine ya grinder nusura kukata uume

Mfanyabiashara mmoja amefichua wakati sehemu ya kifaa cha umeme ilivunjika na kukaa kwenye suruali yake, karibia kumkosesha uume wake.

Mtumizi huo wa mtandao wa TikTok kwa jina Alastair Candlin, kutoka Queensland, alikuwa akitumia mashine ya grinder pembeni siku ya Jumatatu alipokuwa akifanya kazi kwenye mradi nyumbani wakati sehemu ya diski ya chuma ilipopasuka na kurudi nyuma kuelekea kwenye kinena chake.

Katika klipu ya TikTok, mtunzi huyo aliyeonekana na sura ya kuogopa aligeukia kamera muda mfupi baada ya kutokea.

"Ilipovunjika ilitokea haraka sana, nilikuwa nikitafuta ilipoenda. Kidogo tu nipoteze uume wangu," Bw Candlin aliandika kwenye TikTok.

"Nilipotazama chini niliweza kuiona mahali pa mwisho ambapo ningeitaka," alisema.

Kwa bahati nzuri, mashine hiyo ya grinder ilikuwa imetoboa tundu ndogo kwenye nguo zake.

Watazamaji waliopigwa na bumbuwazi walisema jamaa huyo alitokewa na kitendo kilichotajwa kuwa cha bahati sana.

'Mpatie mtu huyu tikiti ya bahati nasibu,' mtumiaji mmoja aliandika.

'Nunua 10 na umpige mtu wa kasino!' mwingine akasema.

Lakini watoa maoni wengine walisema anapaswa kuwa mwangalifu zaidi.

'Nani anakaa hivyo na anatumia mashine ya grinder,' mmoja alisema.

Mwingine aliandika: 'Mambo kama haya hayafanyiki unapotumia kifaa cha kujilinda.'

‘Mashine za grinder, huja na kifaa cha ulinzi kwa sababu hii,' wa tatu aliongeza.

Bw Candlin alisema diski hiyo ilikuwa imechakaa ingawa haukupita muda mrefu tangu anunue mashine hiyo.

"Disc kwenye mashine ya kusagia ilikuwa inazeeka kidogo na ilikuwa inakaribia mwisho wa maisha yake," alisema.

Bw Candlin alisema kuwa aliweka mlinzi kwenye diski kufuatia tukio hilo la kutisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved